HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

23 May 2013

MTAGWA ANGEKUA MMBUNGE ANGESHAPELEKWA INDIA SIKU NYINGI!!!

 

  Naaam wengi wa vijana wa sasa hawawajui nyota waliowahi kutesa katika medani ya soka ya Tanzania kwenye miaka ya sabini hadi mwanzoni mwa themanini basi huwezi kuacha kulitaja jina la Jellah Mtagwa nyota wa zamani klabu za Yanga, Pan African na Taifa Stars.
Nahodha huyo wa kikosi cha Stars kilichoshiriki kwa mara ya kwanza fainali za Mataifa ya Afrika nchini Nigeria mwaka 1980 bado hali yake ni mbaya tangu alipopata ugonjwa wa kiharusi miaka minne iliyopita.
Ukimwona alivyo Mtagwa kwa sasa na maisha anayoishi kwa hakika hauwezi kusema kuwa huyu ndiye ambaye picha zake zilitumika kwenye Stempu pamoja na kuteingenezea nchi heshima ambayo hadi sasa imeshindwa kufikia kwa zaidi ya miaka 30 sasa. 

Kutokana na ugonjwa huo wa kiharusi, Mtagwa hana tena uwezo wa kufanya kazi ya aina yoyote ya kumwezesha kupata kipato cha kukidhi mahitaji yake ya kila siku jambo linalomfanya kuwa kama omba omba kwa kutegemea msaada.
.
'
Ukitazama hata wachezaji nguli duniani hakuna aliyeapata kuwekwa kwenye stamp za nchi yake hata mmoja ukiacha Jellah Mtagwa lakini leo nawaambia hivi Jelahh Mtagwa angekuwa Mbunge na hata asichangie hoja Bungeni hata kama angeumwa jicho wangeshampeleka india kutibiwa lakini kwakuwa ni mcheza mpira anaonekana hana maana yoyote kwa taifa taarifa za kuumwa hazijaanza leo kusikika kuwa anaumwa mbona wengine wakiumwa hata tumbo la kuhara wanapelekwa India kutibiwa .
 
 ''.Mtagwa anasema
''Sio TFF wala Yanga au Pan African au Serikali  ambazo zimewahi kunisaidia, lakini kubwa zaidi namshukuru Mungu kwa kile kidogo anachowajalia baadhi ya rafiki zangu nao hunikumbuka kwa kunilipia matibabu na wakati mwiningine fedha za kunisaidia chakula hapa nyumbani.
''Vilevile hata leo hii mambo si mazuri kiuchumi mpaka sasa bado sijatia kitu chochote kinywani kwangu, lakini nashukuru Mungu kwa kila jambo linalotokea mbele yangu na ninaamini ipo siku nitarejea katika hali yangu ya kawaida,''  Mtagwa.
 
Hivi mpaka mtagwa anatoa maneno haya kinywani mwake viongozi hamsiskii hamuoni kama hizi ni lana za kujitakia wenyewe kwa upande mwingine mungu anaweza kutuadhibu kwa jambo dogo kama hili .
Tanzania Inataka kucheza kombe la Dunia lakini  haitaweza kushiriki kombe la dunia kamwe kama haitamtibia Mtagwa mungu amempa siri Mtagwa ya kufuzu fainali ya kombe la Dunia lakini Mmemtupa mnamuona kinyaa wiki nilikuwa natazama bunge baadhi ya wabunge walivyokuwa wanachangia kuhusu Mtagwa inaonyesha kabisa wanazungumza tu nawaelezeni ukweli hata machafuko yanayotokea Mtwara na baadhi ya sehemu za tanzania ni kwa sababu ya baadhi ya watu kukosa hutu na kuwasahau watu walioliletea taifa sifa na kuwatupa hutafikili ganda la mua au embe .
.

''.
.
Taarifa kwa Wadau wote wa soka Tanzania
Bwana Jellah A Mtagwa ni mchezaji wa zamani wa Pan Afrika, Yanga na aliyekuwa Nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars'' ambaye kwa sasa amepatwa na matatizo ya kiharusi (Stroke) hivyo kumfanya awe mlemavu wa mkono na mguu.
.



No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers