Kwa hakika hivi vimekuwa vikosi Bora zaidi Hasa unapuzungumzia XI Bora za Sir Alex Ferguson ambavyo amewahi kuvipanga kiwanjani .
Huwezi kupingana nae wala kuongeza jambo katika hili ,Ukianza Na mlinda mlango mahili kiwanjani ambaye alikuwa mkali kiwanjani
Peter Schmeichel. ambapo mbele yake akiwa na ukuta imara ambao ulikuwa ukiongozwa na , Gary Pallister na Steve Bruce ambao walitengeneza maelewano mazuri sana kiwanjani , ukuta ambao mwandishi wa makala hii anasema haujawahi kutokea .anasema mbali ya hapo sehemu ya kiungo ilikuwa hatari zaidi kwani kulikuwa na kijana hatari Paul Ince ambaye tulikuwa nyuma yake alikuwa anajua nini cha kufanya kiwanjani .
Mark Hughes alikuwa hatari zaidi kwani alikuwa na miguu yenye nguvu zaidi na alikuwa na uwezo wa kuchukua mipira huku pembeni akiwa na kijana mfaransa Eric Cantona’s ambae alikuwa na uwezo wa hali ya juu katika kupiga chenga na kumiliki mpira kikosi kilimaliza ukata wa miaka 26 kutoka bila kikombe
1995-1999: VIKOMBE VITATU
Miaka michache iliyofuata timu ilibadilika na Ferg alitengeneza vijana wenye vipaji vya aina yake kama Gary Neville, David Beckham, Paul
Scholes na Nicky Butt ambao waliungana na Giggs . hapo ulikuwa lazima uchanganyikiwe kwani katikati mwa kikosi hicho palikuwa na
Roy Keane na Scholes ilibidi ukubali upekee wa sehemu ya kiungo wa wachezaji hawa kwani walitengeneza timu ya aina yake lakini timu hiyo ilikuwa na wachezaji wawili mapacha hatari zadi ambao unaweza kufikili kuwa walikuwa wamezaliwa siku moja au pamoja lakini sio kweli kwani mmoja ni raia wa uingereza na mwingine anatoka visiwa vya kule caribean tunawazungumzia , Andy Cole na Dwight Yorke ambao walitengeneza seshemu kali zaidi ya ushambuliaji .
Teddy Sheringham na Ole Gunnar Solskjaer na kijana kutoka Tobago walidhihirisha , bila shaka , siku ambayo waliushangaza ulimwengu baada ya kufunga mabao mawili na kuimaliza Bayern Munich na kushinda ligi ya mabingwa ulaya mwaka 1999 .
Kwa wakati huo Schmeichel alichaguliwa na kujulikana kuwa ndiye mlinda mlango bora zaidi ulimwenguni .hakika hata nje ya kiwanja kwa maana ya benchi la akiba kulikuwa na vijana kama Jaap Stam,kijana hatari zaidi ambaye alikuwa tayari . hakuwa peke yake Ronny Johnsen,
Henning Berg au Wes Brown wakiwa pamoja , Mholanzi huyo , hakika ulikuwa huwezi kushinda makombe kama haukuwa na kikosi kama hicho .
2006-09 Mwaka wa mafanikio tena ulaya
Baada ya miaka miinne bila ubingwa wa Ligi ya uingereza alitengeneza kikosi kingine ambacho kilikuwa na wachezaji bora zaidi lakini hawakulingana sana na wale wa mwanzo na alikuja na mfumo wa 4-4-2.
,alinunua wachezaji kadhaa ambao waliweza kukabiliana na mfumo wake pamoja na Cristiano Ronaldo, aliweza kushabihiana na Wayne
Rooney na aliongezeka kijana mwingine mwenye nguvu Carlos Tévez ambao walifanya kazi kubwa zaidi kiwanjani .kikosi hiki kiliweza kutwa ubingwa wa ulaya katika fainali iliyochezwa kule
Moscow dhidi ya Chelsea. Baada ya Schmeichel,walipita walinda milango wengi lakini Edwin van der
Sar alipokuja mholanzi huyu ailipata raha golini kwani alikuwa akisaidiwa na ukuta bora ambao ulikuwa ukiongozwa na Rio Ferdinand na Nemanja Vidic ,
Ferguson aliendelea kujikusanyia nishani katika soka . mzee alikuwa akijivunia kundi la watu shupavu . Giggs, Nani na Ji-Sung Park ambaye alisaidiwa na Dimitar Berbatov ambaye alisajiriwa kuongeza radha tofauti katika nafasi ya ushambuliaji
2012-13 Kizazi kipya
Ferguson anakielezea kikosi chake cha sasa kuwa kina uwezo wakufanya mambo makubwa zaidi siku za usoni kikiwa na wachezaji wadogo zaidi kama akina David De Gea, Phil Jones, Chris Smalling, Rafael, Danny Welbeck na Tom
Cleverley – wakiwa chini ya miaka 24 wakiwa na mengi ya kujifunza .
Lakini anaweza kuwa chagua. Jones na Smalling, Bila shaka ,Wanauwezo wa kupigana na kuuonyesha ulimwengu kuwa watakuwa mabeki bora katika safu ya ulinzi ya katika miaka ijayo .
Kutoka na Umri wa Ferdinand’ na majeruhi yasiyokwisha na bila kusahau matatizo kama hayo yanamkabili pia Vidic, muda wao wa kuwepo klabuni hapo unawaka kwa taa ya nyekundu . Kwa sasa, Jones anastahili nafasi katika kikosi manchester united bado ina hazina kubwa sana ya kujivunia hasa katika soka kwani huwezi kuacha kusema kutakuwaje msimu ujao pale wachezaji kama Zaha, Van persie ,Shinji kagawa na wengine ambao unawafahamu watakapo ungana na David Moyes je kitashuka au kitapanda
.
Na mwisho ...Hiki ndio kikosi bora kwetu
Fergie XI
No comments:
Post a Comment