Arjen Robben Anasema kuwa goli alilofunga katika fainali ya klabu bingwa ya ulaya dhidi ya Borussia Dortmund limkumbusha mambo mengi sana katika miaka ya nyuma ya maisha ya soka yake Kijana huyo mwenye miaka 29 alipoteza fainali mbili dhidi ya Inter milan na chelsea na mbaya zaidi kukosa pernaty dhidi ya chelsea katika uwanja wa nyumbani na kwenda kushinda katika uwanja wa wembley .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa uholanzi alikuwa moja kati ya wachezaji ambao timu yake ilifungwa katika fainali zakombe la dunia dhidi ya uispania mwaka 2010 nchini afrika kusini
"Huwezi kutaka uwe katika kundi la watu waliofungwa ," anasema kijana huyo baada ya ushindi wa Bayern' dhidi ya Dortmundu 2-1.
"Tulikuwa na majonzi sana msimu uliopita lakini binafsi niliumia zaidi kwani nilifungwa pia mchezo wa fainali ya kombe la dunia dhidi ya uispani na ni bahati kucheza fanali tatu ..
"sikuogopa sana . Nilijaribu kujiweka katika mfumo chanya wa kuwa naweza kupata nguvu ya kufanya jambo kiwanjani . Sikuanza kufikilia upande hasi ,Bila hivyo ingekuwa ngumu sana .
"Usiku wa jana nimefunga goli . Tumefanikiwa kufanya hilo na sasa tunaweza kusahau mambo mengine ."
Bayern walipata goli la kuongoza baada ya
Robben kumpatia pasi ya aina yake mshambuliaji Mario Mandzukic na kufunga goli hilo .
Dortmund walisawazisha pale Ilkay Gundogan alipofunga kwa penarty baada ya Dante kumfanyia Marco Reus lakini Robben's alifunga katika dakika 89th- na kuipa Bayern ushindi .
Kocha wa Bayern Jupp Heynckes alikubali kuwa kipindi cha kwanza hawakupewa nafasi yoyote ya kuondoka na ushindi lakini mabadilko ya kipindi cha pili yaliifanyika Bayern kuibuka tena na ushindi pasipo kutegemewa
Bayern watakuwa kiwanjani wiki ijayo kuwania kombe la Ujerumani na kama watatwaa kombe hilo basi watakuwa wamechukuwa vikombe vitatu msmu huu .
"Beki wa kulia wa
Bayern ambaye ni nahondha wa Ujerumany Philipp Lahm amekubali kuwa kufungwa katika fainli mbili zilizo pita kuliwafanya wakaze mguu kiwanjani .
"
"
No comments:
Post a Comment