HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

5 September 2012

Zenit St Petersburg Yatumia £64m kuwanunua Hulk na Witsel



Hulk

Mshabuliaji wa Brazil  Hulk, Ambaye alifanya mazungumzo na klabu ya Chelsea ya uingereza Mwezi may Amejiunga na klabu ya soka ya  Zenit St Petersburg akitokea  Porto kwa  ada ya uhamisho wa Euro  £32m.kijana huyo mwenye miaka 26 amesaini kandarasi ya miaka mitano na mabingwa wa Urusi  ambao wanamilikiwa na Luciano  Spalletti.
Zenit imekamilisha pia usajiri wa kiungo  Axel Witsel, 23, kutoka  Benfica kwa ada hiyo hiyo ,Hulk amesema kuwa alikuwa ana raha sana alipokuwa ureno na anataka kuwa na raha pia huko Urusi 

Witsel, amecheza Mechi  30 na timu ya taifa ya Ubeligi  , alianza kuchezea  Standard Liege.
  kama ilivyokuwa  kwa Hulk, na yeye vile vile naye ametia  saini kandarasi ya miaka mitano na klabu hiyohiyo

Hulk,anaweza kucheza pia kama winga  , aliwahi kufanya mazungumzo na  Roberto Di Matteo' wa  Chelsea mara baada ya   Didier Drogba alipotangaza kuondoka stanford bridge hasa baada ya timu hiyo kushinda ligi ya mabingwa Dhidi ya Bayern Munich Hulk alijiunga na porto akitokea Verdy ya japan 2008 na alifunga magoli 54 katika mechi 103 za ligi

Hulk,ni moja kati ya wachezaji walikuwemo kwenye kikosi cha Brazil wakati wa mashindano ya olimpick wakati wa kiangazi   Witsel ataanza kazi dhidi ya malaga katika ligi ya mabingwa barani ulaya sept 18 ambapo wapo kundi moja na  AC Milan and Anderlecht.


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers