Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri , Mohamed Abu Treika, anatarajia kurudi nchini kwao misri katika klabu ya , Al Ahly baada ya kumaliza mwaka mmjoa wa mkopo huko UAE.
“Nitarudi nyumbani kwetu baada ya kumaliza mkataba wangu wa mkopo msimu huu japokuwa naskia vizuri kukaa hapa lakini nataka kurudi nyumbani na kwa mashabiki wangu” .
Mchezaji huyo mwenye miaka 34-amecheza kwa miezi sita katika timu ya falme za kiarabu UAE Abu Dhabi timu inayojilikana kama Bani Yas’ na kuisaidia timu hiyo kushinda kwa mara ya kwanza kombe la ligi kuu ya nchi hiyo GCC League .
Kwanini uliamua kuondoka katika klabu ya wazazi wako ?
“Nilikuwa na sababu zilizonifanya niondoke Al Ahly wakati wa baridi na sababu zenyewe zimekwisha malizika ,” .
Mchezaji huyo alifunga goli katika siku ambayo aliagwa yaani jana dhidi ya Al Khor ya Qatar.
“Ninafuraha kuondoka Bani Yas ambayo imeshinda GCC taji la lao kwanza msimu huu ,”.
No comments:
Post a Comment