Kikosi cha timu ya
Small Simba cha miaka ya tisini na themanini ambacho licha ya kuonesha kandanda la uhakika
na kuvutia pia kilikuwa mwiba kwa timu za Simba na Yanga.
Wapenzi na Wanachama wote waanzilishi wa iliyokuwa Klabu Maarufu ya mchezo wa soka hapa Zanzibar Timu ya kandanda ya Small Simba wanatarajiwa kukutana kesho asubuhi katika azma ya kutaka kuifufua tena Timu hiyo.
Wapenzi na Wanachama wote waanzilishi wa iliyokuwa Klabu Maarufu ya mchezo wa soka hapa Zanzibar Timu ya kandanda ya Small Simba wanatarajiwa kukutana kesho asubuhi katika azma ya kutaka kuifufua tena Timu hiyo.
Kikao cha kutafakari
mustakabali wa timu hiyo kinatazamiwa kuwa wazi kikikaribisha pia wadau
wa klabu hiyo ambacho kitafanyika katika jengo la CCM la Jimbo la
Kikwajuni liliopo hapo mnazi Mmoja Mjini Zanzibar majira ya saa 3.00 za
asubuhi.
Akikaririwa na vyombo
vya Habari Mmoja wa waanzilishi wa Klabu hiyo maarufu katika miaka ya
1980 na 90 Dr. Juma Mambi kwa niaba ya Katibu mteule wa Klabu hiyo
Kassim Juma alisema mada tatu zitajadiliwa katika kikao hicho.
Dr. Mambi alizitaja
mada hizo kuwa ni pamoja na Kujua mustakabali wa Small Simba, kufufua
ari na hamasa za wapenzi wa Klabu hiyo pamoja na mengineyo
yatakayojichomoza katika kikao hicho.
Dr. Mambi aliwaomba
pia wana habari kushiriki katika kikao hicho lengo la kutafuta mbinu na
njia ya kutaka kurejesha ari na hamasa ya mchezo wa soka ambao ulikuwa
katika kiwango cha juu wakati timu hiyo ikiwa katika Nyanja za
Kimichezo.
Timu ya Soka ya Small
Simba iliwahi kushika ubingwa na soka wa daraja la kwanza hapa Zanzibar
na kutoa upinzani mkali kwa timu za Yanga na Simba za Dar es salaam
katika iliyokuwa mashindano ya klabu bingwa ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment