Marehemu
alitambulika sana katika tasnia ya muziki kupitia wimbo wa GETO LANGU
TU na baadae alirekodi nyimbo nyingi zilizopendwa na jamii ya
watanzania.
Tunawaomba
watanzania wazidi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu,
Shirikisho lenu lipo imara na tunashiriki kikamilifu katika msiba huu
tukishirikiana na wadau mbali mbali.
Tunapenda
kuwatangazia kuwa Shughuli nzima ya mazishi ya mpendwa wetu ALBERT
MANGWEA zitasimamiwa na Familia ya Marehemu, Shirikisho la Muziki
kupitia chama cha Muziki wa kizazi kipya na wadau mbali mbali.
Kwa
sasa tunakamilisha taratibu zote za awali, maandalizi na ratiba mzima
itatoka baadae. Tulifanya kikao na kaka wa marehemu (KENNETH MANGWEA)
na kukubaliana kuwa msiba utakuwa MBEZI BEACH eneo la GOIG kwa sasa
tunashirikiana vyema katika kukamilisha haya.
Kama
mambo yatakwenda sawa, ikiwa ni pamoja na kuuleta mwili wa marehemu
tunatarajia kuaga siku ya Jumamosi na baadae kusafirisha kwa Shirikisho
la Muziki Tanzania (Tanzania Music Federation) tunasikitika kutangaza
kifo vya msanii ALBERT MANGWEA kilichotokea Afrika ya Kusini akiwa
kwenye shughuli zake za kimuziki . Tunawapa pole Wazazi, ndugu, jamaa na
watanzania wote kwa kuondokewa na mwanamuziki huyo mkongwe wa kizazi
kipya, marehemu tutamkumbuka kwa mengi hasa msimamo aliounesha katika
mambo aliyoyaamini, Alikuwa ni mtu mwenye jitihada hata mauti ilipomkuta
alikua kwenye kujitafutia riziki.shughuli ya
Mazishi huko Morogoro eneo la Kihonda nyumbani kwa mama yake mzazi MAMA
DENISIA MANGWEA.
Tunaomba tushirikiane sote kwa PAMOJA katika katika kipindi hiki kigumu.
Taarifa zaidi tutawapatia baadae kadri itakavyo bidi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe.
Vile
vile tunampa pole mwanamuziki Mgaza Pembe (M TO THE P) na kuomba maombi
ya watanzania kumuombea mwanamuziki huyo ambaye aliyekuwa Afrika
Kusini na Marehemu. M TO THE P amelazwa Afrika Kusini. Tunamuombea apone
haraka.
Addo November Mwasongwe
Raisi Shirikisho la Muziki Tanzania
0713396367/0754396367
29th May 2013.
No comments:
Post a Comment