Rais
Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa
Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa
waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa
Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo
kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Rais
Jakaya Kikwete akiongea na wachezaji wa timu ya mpira ya Taifa, Taifa
Stars leo Ikulu jijini Dar es salaam alipokutana nao kuwapa hamasa
waweze kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Moroco utakaochezwa
Juni 7, na michezo mingine ikiwa ni hatua ya kuiwezesha timu hiyo
kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Rais
Jakaya Kikwete akiwaaga wachezaji wa Timu ya Taifa Stars mara baada ya
kukutana nao leo Ikulu Jijini Dar es salaam kuwahamasisha washinde
mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Moroco utakaofanyika June 7 ikiwa ni
sehemu ya Taifa Stars kutafuta ticketi ya kucheza mashindano ya Kombe la
Dunia.
Meneja
wa Timu ya Taifa Stars Bw. Mukebesi akiteta jambo na Kepteni wa Timu ya
Taifa Stars Juma Kaseja Ikulu jijini Dar es salaam walipokutana na Rais
Jakaya Kikwete.
Wachezaji
wa Timu ya Taifa Stars wakipata chakula walichoandaliwa na Rais Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo alipokutana nao kuwatakia ushindi
katika mchezo wao dhidi ya Moroco.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na wachezaji wa Timu ya
Taifa , Taifa Stars, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na
Michezo na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa , Taifa Stars Ikulu jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO na Freddy Maro Ikulu.
Na Veronica Kazimoto –MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo
amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika
mechi ijayo dhidi ya timu ya taifa ya Moroco mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil .
Rais
Kikwete amewaambia wachezaji wa timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele
kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao dhidi ya Gambia
ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0.
“Maadamu
mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi
dhidi ya Moroco, mkishinda tutafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea
sana,” Kikwete.
Aidha
amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen pamoja na Kamati ya Taifa
ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi
milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia na
kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi
sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.
Kwa
upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na
kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili
kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.
Akizungumza
kwa niaba ya wachezaji wenzake nahoidha wa timu hiyo Juma Kaseja
amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye
kuibuka washindi kwenye mechi zijazo.
Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment