Rais wa chama cha soka cha Burundi FA Lydia Nsekera amechaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza katika kamati kuu ya fifa na kuvunja rekodi ya miaka 109 .
Nsekera, 46, atahudumu kwa miaka minne baada ya kushinda katika kura zilizopigwa katika mkutano mkuu wa fifa huko Mauritius.
Nsekera alikusanya kura 95 kati ya mia mbili na tatu 203 akiwazidi kete wakuu wa soka la Australian Moya Dodd na Sonia Bien-Aime, kutoka Uturuki na visiwa vya Caicos.
Nsekera anasema : "Nitawachagiza wanawake waamini kuwa wanaweza kuongoza na nitawaunga mkono wanawake wote katika vyama vya soka ."
Nsekera,ambaye mwaka jana alipendekezwa kuchaguliwa kugombea katika kamati kuu ,ameliongoza shirikilisho la soka la Burundi Tangu 2004 na alikuwa mwanachama kamati ya maandalizi ya mashindano ya 2008 na 2012 .
akiwa kama mwanachama wa maandalizi ya olimpick pia alikuwa katika kamati huru ya kuzuia rushwa mwaka 2011 .
Nsekera ameimbia BBC: "Ninafuraha sana kuwa mwanamke wa kwanza ni jambo muhimu kwa afrika na ni muhimum pia kwa Burundi na kwa wanawake pia .
No comments:
Post a Comment