Washindi wa nne wa ligi kuu ya Bara, Kagera Sugar wamesema hawana mpango
wa kusajili wachezaji wa kigeni na kwamba wapo kwenye mazungumzo na
wachezaji ambao mikataba yao imemalizika kwa lengo la kuongeza mikataba
hiyo.
kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Mrange Kabange, amesema baada ya kushika nafasi ya nne nyuma ya Yanga, Azam na Simba, wataendelea kuwatumia wachezaji wa msimu uliomalizika.
"Hakuna mchezaji mpya tuliyeanza naye mazungumzo ila uongozi upo kwenye mazungumzo na wachezaji wetu wa zamani ambao wamefanya kazi kubwa kuhakikisha timu inafanya vizuri msimu huu ulioisha," .
Aidha, amesema kuwa uongozi wa timu hiyo upo kwenye mazungumzo ya mwisho na Mganda Jackson Mayanja kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo msimu ujao baada ya Abdallah Kibadeni kujiunga na Simba.
"Baada ya Kibadeni kuondoka, kwa sasa uongozi upo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na Mayanja ambaye aliwahi kuifundisha timu hii kabla ya Kibadeni," .
Pia amesema moja ya mikakati ya timu hiyo kwa sasa ni kukiimarisha kikosi cha timu B kwa ajili ya kuwekeza kwenye soka la vijana ili waje kuwatumia kwenye ligi kuu siku za usoni kama ilivyofanya Simba.
mara baada ya Mayanja kukabidhiwa rasmi timu ataangalia uwezekano wa kupandisha wachezaji kutoka timu B kwa ajili ya msimu ujao.
Kibadeni baada ya kuiwezesha timu kushika nafasi ya nne kwenye ligi ameiacha na kujiunga na Simba kuchukua nafasi ya kocha Mfaransa, Patrick Liewing ambaye ajira yake imesitishwa katika timu hiyo iliyoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

No comments:
Post a Comment