Habari msomaji wangu leo nilikuwa na tazama kituo cha
runinga cha StarTv katika Kipindi cha tuongee Asubuhi leo
walikuwa wamewaalika Msemaji wa shirikisho la soka la Tanzania Tff
Boniphase Wambura Mgoyo na aliyekuwa
Katibu mkuu wa chama hicho zamani FAT na baadae Tff Michael Richard Wambura.
Bila shaka kwa majina haya niliyokutajia wote hawa watakuwa wenyeji wa Mkoa wa Mara mkoa ambao unasifika zaidi kwa kutumia nguvu nyingi akili kidogo hasa kwa` wakazi wa mkoa huo lakini hawa hawako hivyo wawili hawa hutumia akili nyingi kujadiri mambo kwa hoja.
Bila shaka kwa majina haya niliyokutajia wote hawa watakuwa wenyeji wa Mkoa wa Mara mkoa ambao unasifika zaidi kwa kutumia nguvu nyingi akili kidogo hasa kwa` wakazi wa mkoa huo lakini hawa hawako hivyo wawili hawa hutumia akili nyingi kujadiri mambo kwa hoja.
Naanza na Michael Wambura
kiukweli moja kati ya watu ambao wanaweza kuchukiwa na kuonekana wa baya katika
soka la Tanzania ni Wambura ambaye kila utakaposkia kuna chaguzi yoyote inataka
kufanyika hasa katika wakati wa pingamizi na yeye lazima pingamizi lake
litakuwemo Eidha mtu anasifa au kukosewa kwa kanuni au sheria au badiliko
lolote la kikatiba la tff au chama
chochote cha soka.
Hapo ndipo hukera watu wengine ambao
wanamtazamo tofauti na yeye katika swala zima la kanuni lakini wakati natazama
kipindi kile Tom chilala mtangazaji wa kipindi hicho ambaye alikuwa akisimamia
kipindi kwa upande wa Dar Es –Salaam alimuuliza swali Michael Wambura kuhusu
Udhamini wa michezo Mbalimbali katika soka la Tanzania bila kujari ligi au mashindano ya vijana .
Wambura akaanza kujibu Kwanza
alinijibu swali ambalo siku yoyote kama ningekutana na watu wa TBL ningewauliza lakini
yeye akanijibu kisomi zaidi alianza kunibadili kimtazamo sana kwa kusema TBL
haina makosa kudhamini Timu ya soka taifa ya Tanzania yaani taifa stars kwa
sababu ndiko mahala pake licha kuwa inatumia pesa nyingi kwenye timu ambayo haina
tija .
Akasema TBL haiwezi kudhamini timu za
vijana kwa sababu kisheria hairusiwi kufanya hivyo kwa sababu hata pombe
yenyewe watoto hawarusiwi kunywa sembuse kudhamini wambura akaendelea kusema hata hizo kampuni zinzodhamini michuano ya watoto ambayo TBL inashindwa haifanyi hivyo kwa
kiwango stahili akatoa mfano kuwa Baadhi ya kampuni moja ambayo hudhamini mashindano ya hayo inatoa shilingi laki mbili kundesha
ligi ya za michuano hiyo kwa vijana kitu ambacho kwa mikoani si pesa kabisa hasa
katika soka la Tanzania kwani hata pesa kwa Dar Es salaam kwa pesa hiyo hata kwa nauli haitoshi bado kunatakiwa kutazamwa upya katika swala la
udhamini .
Nilivutiwa sana na wambura kwani
ukitazama kwa pesa aliyoitaja sipesa ya kundeshea programe za vijana tena
akaweka na msisitizo kuwa mashindano
hayo ambayo huchezwa mara moja kwa mwaka kiukweli kwa alichokizungumza wambura
ni tofauti na vile nilivyokuwa nikimfikiria siku zote hapa aliongea kisoka zaidi tena kwa jicho la
mbali hata mimi namuunga mkono Michael wambura ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa simba yakati fulani kwakweli vile
nilivyokuwa nikimtazama na kumchambua sasa imekuwa tofauti kidogo alinikuna kwa
kuongea mambo ya msingi katika soka .
Wambura akaulizwa tena na Tom mwana
wa Chilala kuhusu mustakbari wa soka la Tanzania na matarajio ya timu ya soka
ya taifa kuhusu mashindano ya kombe la CHAN mashindano yanahusisha wachezaji
wanaocheza ligi za ndani
Wambura anasema kuwa shida ya
Tanzania huwa inataka kuonekana ipo wakati mipango ya soka haipo anasema kuwa ukitazama vizuri mechi ya
Tanzania na Uganda ya kwenda Chan ,tayari Uganda inanafasi kubwa zaidi kwani
ukitazama kwa upande mwingine timu yoyote ile Duniani inapokwenda kucheza
Ugenini huwa inajaribu kufanikisha mambo yafautayo Eidha kutoa suluhu au
kutoruhusu magoli mengi ya kufungwa lakini wao Uganda walishatufunga hapa kwetu
kwake yeye tayari mechi ishakwisha kwani itakuwa ngumu kushinda mechi na Uganda
katika uwanja wao.
Ila akasema kitu pekee kitakachoweza
kuifanya Tanzania kushinda mechi hiyo ni kuweka akili yao katika soka ya kisomi yaani professionalism akiwa na maana ya bila kujari idadi ya mashabiki wa uganda
watakuwa wangapi kiwanjani, wao wanachotakiwa kujari ni kwamba mashabiki hao
hawachezi wanaocheza ni wachezaji ndio
maana hata tembo wa ivory coast walitufunga kwa sababu wao walifanya kama
alichosema
Kama kawaida ya wambura hakuacha
kuponda michuano hiyo ambayo watanzania wengi ndiyo imebaki kuwa tumaini lao
lakini akasema ya kuwa`mashindano hayo nchi nyingi zilizo endelea zimekuwa
zikichukua wachezaji wa majaribio japokuwa nao huwa sio wa kulipwa ndio maana
nchi kubwa kisoka za afrika hazitilii maanani michuano hiyo kwa sababu kubwa
kuwa haitambuliki na fifa kwa hiyo hata wasipo shiriki haiathiri jambo lolote
hapa ukitazama wambura anakuja na hoja ya msingi kidogo.
Lakini ukitazama ni kama anaipiga
kijemmbe shirikisho la soka la Afrika CAF wambura akajibu swali jingine kuhusu
tiba ya michezo sehemu ambayo kwa afrika ni jambo ambalo halitiliwi mkazo sana
kwasababu ya kutopewa kipaumbele hasa na wachezaji kuumia na kutopewa tathimini
ya kutosha matokeo yake huishiwa kupigwa Ganzi kila uchao na kufika kipindi
majeraha kukithiri mwilini na hivyo kujikuta mchezaji akiwa na umri mdogo
kukimbilia kucheza veteran anasema ukitazama waganga wanaotibu wachezaji katika
timu husika hawazidi nane kitaaluma wakati mwingine mganga huyo huyo mmoja kuajiriwa mara
mbili klabuni na timu ya taifa sasa je Timu za mikoani wako wangapi ?
Aliniacha hoi bin Taaban kwa yake
aliyoyasema kwani alizungumza ukweli mtupu kuhusu jambo hilo nilipunguza hasira
zangu kwa yale aliyofanya nyuma kimtazamamo na inawezekana kuwa Wambura
anazungumza mambo ya kimsingi lakini na yeye ni mwandamu anaweza kuwa na
mapungufu yake ndo maana amebarikiwa kuweka pingamizi si ajabu anaweza kufanikiwa
mara baada ya katiba ya tff kubadilishwa
au kufanyiwa marekebisho maana sisi wengine sio watalaamu kisheria japokuwa
yanaweza ya kamkuta tena kwani hizo kamati zitafuata kanuni zile zile ambazo
mwanzo zilikuwa zikimtoa nishai .
Namaliza na msemaji wa shirikisho
ambaye yeye aliyongumza kuhusiana na
timu na mandalizi na maendeleo ya kambi ya timu ya taifa japokuwa kuna wakati Abdallah Tilata alimchokoza kwa kumuuliza vp kuhusu Athumani Iddy kuikacha timu ya taifa
na baadae anaonekana kufanya mazoezi na timu mwanza tena kwa hari ya juu
Waambura anasema kuwa Athumani iddy bado yupo timu ya taifa na muda ukifika pale
atakapoona inafaa ataandika barua ya kustaafu timu ya taifa ili aongeze`nguvu
timu yake anayochezea klabuni.
No comments:
Post a Comment