Quinton Fortune, Mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa
anasomea fani ya ualimu wa soka kwenye kompaundi ya Manchester United
alipotembelea Azam FC Chamazi leo kwa mwaliko wa DHL
Fortune alishangazwa na ubora wa Center ya Azam FC na kusema hajawahi kuona kitu kama hiki kinachomilikiwa na klabu hata kwenye nchi yake ya Afrika ya Kusini Hakuna..
Fortune alishangazwa na ubora wa Center ya Azam FC na kusema hajawahi kuona kitu kama hiki kinachomilikiwa na klabu hata kwenye nchi yake ya Afrika ya Kusini Hakuna..
Kauli hii ya fortune hainishangazi labda jambo ambalo lingenishangza kama angeenda kuziona zile klabu zangu mbili zinazo pigizana kelele utafikili wapo kwenye uchuuzi wa samaki pale feri au kariakoo
Klabu hii za Azam ambayo nakumbuka wakati ikitafuta kupanda daraja kuna wakati nilikuwa nakutana na gari yao maeneo ya kigogo lakini sasa napishana na mabasi makubwa .
Hili ni jambo la kujivunia kwa sababu Leo nilipata bahati kubwa ya kuzungumza na jaffar Iddy alikuwa akinieleza kile ambacho Fortune aliwaambia kuwa ata yeye mwenyewe wakati anaingia Man utd Hakuamini lakini aliawaeleza wchezaji wa Azam walipata nafasi ya kumuuliza maswali na mengi lakini cha msingi ni kuwa Azam fc walimfurahia zaidi , Jaffar Iddy kwa kua anatoka Bara la Afrika na ametembelea klabu hiyo ambayo wakati anachezea Man u
Azam Fc haikuwepo pengine ilikuewepo kwenye makalatasi lakini alipoondoka Man u Azam fc ilianza kuonyesha Dalili za kuonekana.
Yapo mambo mengi ambayo Fortune ameyaona Azam fc na kudiliki kusema kuwa hata Nchini kwake hakuna klabu inayofanya jambo kama hilo kiasi cha kuuliza kuwa hii timu ni ya mtu au ya wanakikijiji
lakini ni ya mtu Binafsi jambo lililomfanya achanganyikiwe zaidi.
Hivi tugeuze kiswahili kwa mfanooo Teh teh teh angekwenda simba ingekuaje nafikili angekutana na haya :- jambo la Kwanza kuruka viunzi vya nyanya zinauzwa pembeni ya klabu hiyo kelele za honi za magari harufu mbaya za mitalo iliyokithiri kwa harufu mbaya ambazo hata mbuzi hawezi kustaamiri kunusa Bila kusahau matusi ya Nguoni kutoka kwa wachuuzi wadogo wadogo wa simu na kelele za majenetreta ya umeme yanayo pambana na mgao usio kwisha katika mmtaa wa Agrey .
Kwenye Jengo sasa Kidogo Mh Mbunge angeweza kujitetea kuwa aliichukua klabu ikiwa katika
Hari mbaya na sasa anafanya marekebisho kwani unapoaingia getini katika klabu ya simba jengo la mkono wa kulia ndio linalo oonekana lina uafadhari la mkono wa kushoto sasa sina hata haja ya kulizungumzia lakini sijapita siku nyingi kwa kuogopa mafua yasiyo tibika inawezekana wametengeneza japo nakuwa Toamaso katika swala hilo.
Sasa shughuri na majibu ya kigugumuzi ingekuwa hapa Fortune angeomba kwenda kuona Academy na uwanja wa kufanyia mazoezi ya simba majibu yangekuwa hapa hivi
Kimombo (Yah Fortune You know ,,yeah the the stadium is is very Problem from hear i mean far away) majibu mengi ya kujigonga gonga sema tu hatuna kiwanja baba .
Lakini Fortune Huyu huyu kama angeenda Yanga yaani maskani ya klabu ya yanga kule mtaa wa twiga na jangwani angeweza kukutana na mipango isiyokwisha na iliyojaa siasa nyingi bila shaka angekutana GYM ambayo bado tunamashaka kama inafanya kazi mpaka sasa kiofisi sio haba lakini Academy hakuna pengine wangemuonyesha uwanja wao ambao wanashindwa hata kumwagilia maji ili uote nyasi.
Bila shaka Fortune atakaporejea Manchester kuendelea na masomo ataikumbuka Azam fc na kuifurahia na huenda siku zijazo ubingwa wa Tanzania unaweza kuelekea mbagala .
Jambo kuu na la kipekee Azam fc inaifanya timu hii ionekane kama iko ulaya wakati iko Tanzania tena mbagala maeneo ya Chamazi na nina Diliki kusema na kukubali msemo wa kitabu ninacho kiamini cha Biblia kuwa wale walio kuwa wa kwanza watakuwa wa mwisho na wale walio kuwa wa mwsiho watakuwa wa kwanza
Hiki ndio kifo Cha Simba na Yanga Well Done Azam fc
No comments:
Post a Comment