Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF),
Sunday Kayuni
atashiriki warsha ya
wakufunzi
wa
makocha wa Shirikisho
la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF)
itakayofanyika
kuanzia Oktoba 22-24
mwaka huu.
Warsha hiyo
iliyoandaliwa na
CAF kwa ajili ya wakufunzi wake
itafanyika nchini Cameroon.
Wakufunzi 18 wa CAF kwa upande wa makocha watahudhuria
warsha hiyo.
Madhumuni ya warsha hiyo
ni kuainisha majukumu yao,
kubadilishana uzoefu.
Pia kuwapa methodolojia mpya ya ufundishaji na
muongozo kuhusu mfumo wa leseni za makocha
ambao watautumia katika nchi wanazotoka.
Mbali ya Kayuni Tanzania,
wakufunzi wengine ni Ahmed Babiker
(Sudan), Amadou Shaibu (Nigeria),
Boy Bizzah Mkhonta (Swaziland),
Duodu Fred Osam (Ghana), Edussei
Anthony (Ghana), Fathi Nossir
(Misri), Faouzy Altaisha (Sudan)
na Fran Hilton Smith (Afrika Kusini).
Wengine ni Francis Oti-Akenteng
(Ghana), Honour Janza (Zambia),
Kasimawo Laloko (Nigeria),
Mahmoud Saad (Misri), Paul
Hamilton (Nigeria), Serame
Letsoaka (Afrika Kusini),
Shawky Abdel Shafy (Misri),
Thondoo Govinder (Mauritius)
na Ulric Mathiot (Seychelles),
No comments:
Post a Comment