Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinaanza
kesho (Novemba 6 mwaka huu) ambapo Ashanti United itakuwa mwenyeji wa
Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio
katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili chini ya mwamuzi
Andrew Shamba kutoka Pwani ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000. Waamuzi wasaidizi ni Abdallah Mkomwa na Rashid Abdallah wote
kutoka Pwani wakati mezani atakuwa Hamisi Chang’walu.
Mechi
nyingine za kesho ni JKT Ruvu Stars na Coastal Union (Uwanja wa
Chamazi), Kagera Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba) na
Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Keshokutwa
(Novemba 7 mwaka huu) raundi ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza
itakamilika kwa mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa
kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam
itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja
wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
Rhino Rangers na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Novemba
7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa
Tanzania Prisons.
TFF YATAKA ORODHA YA WALIOSAMEHEWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma waraka kwa vyama vya mpira wa
miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha orodha ya
wote waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.
Oktoba
28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu baada ya uchaguzi,
Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa
sababu mbalimbali.
Hata
hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa
au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.
Vyama
vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa wanachama wao
(vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote
waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).
TANZANITE KWENDA MAPUTO KESHO
Kikosi
cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kinaagwa
kesho (Novemba 6 mwaka huu) saa chache kabla ya kuanza safari ya kwenda
Maputo, Msumbiji.
Hafla
fupi ya kuikabidhi bendera Tanzanite itafanyika kesho saa 5 asubuhi
kwenye ofisi za TFF wakati kikosi hicho kinatarajiwa kupaa saa 11 jioni
kwa ndege ya LAM na kuwasili Maputo saa 3.45 usiku.
Msafara
wa Tanzanite ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 10-0 karibu wiki
mbili zilizopita jijini Dar es Salaam utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF, Kidao Wilfred.
Mechi
hiyo ya marudiano itachezwa Novemba 9 mwaka huu Uwanja wa Taifa wa
Zimpeto, na timu itarejea nyumbani Novemba 10 mwaka huu saa 8.30 mchana
kwa ndege ya LAM.
No comments:
Post a Comment