Manchester City imepangwa kukutana na Barcelona katika hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa Bara la ulaya katika hatua ya kumi na sita Bora .huku mahasimu wao
Arsenal wakipangwa tena na Bayern Munich.
RATIBA YA LIGI HIYO
- Michezo ya kwanza itachezwa : 18/19/25/26 February na 11/12/18/19 March (utakuwa Mzunguko wa pili
- Robo fainali : 1/2 April na 8/9 April
- Nusu fainali: 22/23 April and 29/30 April
- Fainali : 24 May
Chelsea,ambao ni mabingwa wa mwaka 2012 watapambana na Galatasaray wakati Manchester United watasafiri hadi Ugiriki kupambana Olympiakos.
Mechi nyingine za Mzunguko huo , AC Milan watakutana na Atletico Madrid, Bayer
Leverkusen watakwenda ufaransa kumenyana na Paris St-Germain, huku Schalke wakiwa na kibarua kigumu cha kuwazuia mabingwa mara tisa wa ulaya Real Madrid na Zenit St
Petersburg itakutana na washindi wa pili wa mwaka jana Borussia Dortmund.
Chelsea na Manchester United wao wanafaida ya kucheza mechi za pili Nyumbani baada ya kuongoza makundi yao wakati ,City
and Arsenal zitacheza Nyumbani mechi za kwanza na kumaliza Ugenini
Mtendaji mkuu wa City Ferran Soriano na Mkurugnzi wa ufundi wa Barca Txiki Begiristain
walikuwa wanafanya kazi pamoja na ndiye aliyemuuza Yaya Toure kwa City mwaka 2010.
Begiristain ameiambia Sky Sports: "Kuna timu mbili kubwa ,Moja ikiwa na historia kubwa ulaya na nyingine inawachezaji wakubwa wanaochipukia .
MECHI WALIZOKUTANA BAINA YA Arsenal na Bayern Munich
14 Mar 2001 - Bayern 1 Arsenal 0
22 Feb 2005 - Bayern 3 Arsenal 1
9 Mar 2005 - Arsenal 1 Bayern 0
19 Feb 2013 - Arsenal 1 Bayern 3
13 Marc 2013 - Bayern 0 Arsenal 2
"Ni timu yenye kujiamini baada ya kushinda dhidi ya mabingwa wa sasa katika uwanja wao wa nyumbani na wakiwa na uzoefu wa kutosha kwa kucheza mara mbili nyumbani na Ugenini Dhidi ya Barcelona .
"Barcelona ni mabingwa mara nyingi zaidi lakini tunajiamini ."
Arsenal
ilishinda 2-0 ugenini Dhidi Bayern Munich Mwezi March lakini iliondolewa kwa sheria ya Goli ugenini baada ya kufungwa mechi ya kwanza 3-1 , huku wajerumani wakienda kucheza fainali na ndugu zao Dortmund.
Bayern wamewahi kuiondoa Gunners mara mbili katika mashindano hayo .
Chelsea itapambana na Mshambuliaji wake wa zamani Didier Drogba kwa mara ya kwanza Tangu raia huyo wa Ivory coast kuondoka Stamford Bridge baada ya kukaa miaka nane 2012.
Kocha Jose Mourinho
alikaririwa juma lililopita kuwa mechi hiyo ndiyo aliyokuwa akiitaka .
RATIBA KAMILI :
Manchester City v Barcelona
Olympiakos v Manchester United
AC Milan v Atletico Madrid
Bayer Leverkusen v Paris St-Germain
Galatasaray v Chelsea
Schalke v Real Madrid
Zenit St Petersburg v Dortmund
Arsenal v Bayern Munich
No comments:
Post a Comment