Moja kati ya Jambo
kubwa katika soka la Tanzania ukiwa kama kocha unalazimika kushinda mechi
iliyopo mbele yako .
Tena ni mtazamo
uliojengeka katika vilabu viwili vya kihistoria Simba na Yanga kwa hakika ni vilabu vyenye ngome imara ambazo
zinatumika visivyo. Wengi wa wanachama
na viongozi wa vilabu hufanya vitu kutokana na matakwa yao Binafsi simba na
yanga ndio vilabu ambavyo vimefundishwa na makocha wengi zaidi wakiwemo wazawa
na wageni :- Katika kichwa changu cha habari cha msingi nimeandika ningekuwa
kuwa kocha wa Kigeni nisinge kuja kufundisha mpira Tanzania tena naongeza hata
kama ningekuwa Napata mshahara anaopata Gareth Bale achana na wa Cristiano Ronaldo !
Lakini kwanini
Nisingekuja kufundisha mpira Tanzania ? hili ndilo swali muhimu na ndilo linalo
hitaji majibu hapa sitataja makocha
wengi lakini nitataja japo kwa kiupekee
Naaam naanza kutoa sababu lakini zaweza kuwa sio za msingi kwa upande
wako hivi karibuni klabu za Simba na Azam zilisitisha mikataba ya makocha wao
kwa kile wanachoamini kuwa hawajafanya yale wanayotaka hadi kufika sasa
yawezekana ikawa kweli au uongo.
Sasa tuanze na simba
ambao wao walimuondoa mfaransa Patrick Liewing na kumpa Abdallah Kibadeni
kuifundisha timu ya simba mpaka nusu msimu simba imeshika nafasi ya nne na
baadhi ya mashabiki na wanachama wakaanza kusema kuwa Kibadeni hafai
kuifundisha simba jambo ambalo haliniingiii akilini kabisa nafasi nne unasemaje
Kibadeni hajui kufundisha wakati anafundisha timu hiyo kwa mara ya kwanza ,
Kibadeni kabla hajaja simba alikuwa akiifundisha Kagera sugar ya Mkoa Kagera
timu ambayo ilikuwa ikitishia usalama wa baadhi ya timu hasa simba yanga
,Mtibwa na Azam apa ndipo alipoonekana Lulu na klabu ya simba kumpa kazi lakini
leo hafai .
Katika makocha wa
Kigeni waliokuja kufundisha mpira Tanzania hakuna kocha hata mmoja aliweza
kukaa zaidi ya Miaka miwili zaidi ya Stewart John Hall wa Azam japo hata yeye
aliwahi kufungishwa vilago ambaye hivi karibuni alifungishwa vilago na klabu hiyo.
Hapa nilikuwa nakupa
mwangaza tu sasa tuje kwenye sababu kuuu
kwanini Nisingefundisha Tanzania
Baada ya kocha wa
Azam kuachia ngazi alipata kuhojiwa na moja kati ya Televisheni moja nchini siitaji jina alisema
haya baada ya kuuliza swali je unafikiri kwanini umeshindwa kutwaa ubingwa wa
Tanzania.
Stewart alijibu
hivi:-Sijashindwa Simba na yanga wapo
hapa Tangu siku nyingi sana kabla hujafanya chochote lazima ufanye utafiti
kwanini hawa wanabadilishana wao Ubingwa tu niligundua yafuatayo katika miaka
yote hakuna siku simba na yanga zimekuwa Katika kiwango Bora zote kwapa pamoja
lazima Mmoja atakuwa juu mmoja atakuwa chini sasa la msingi jaribu kuwa
katikati yao kitu ambacho amefanikiwa
kwa asilimia tisini na lililobaki ni kuutwaa ubingwa ambao pia hautwaliwi
kirahisi hata kidogo.
Sasa ukitazama
mazungumzo ya Stewart karibu sasa utaanza kupata majibu ya kwanini nisingekuja
kufundisha soka Tanzania jambo kuu kuliko yote ni kuwa Vilabu Vingi vya
Tanzania vimekuwa hazina mipango ya muda mrefu wao hutaka kushinda mechi
iliyopo mbele yao hata kama hawawezi kushinda mechi hiyo.
kifupi
kanuni za kufundisha simba na yanga unatakiwa kushinda tuu Epuka kutoa
Suluhu au kufungwa Tena simba au yanga mashabiki
siku zote huwa hawapendi kufungwa lakini wa simba na yanga wamezidi wao kufungwa kwao ni dhambi ukiwa kama kocha hili haliwezekaniki hakuna timu
isiyofungwa Duniani lakini ukiwa kocha wa kigeni hakikisha Hufungwi.
Jambo la pili katitika
tawara kuna kitu kinaitwa Bodi ya
menejimenti au Tawara klabu za simba na yanga ni klabu ambazo kama zimelaaniwa
hivi kiutendaji hakuna siku hata moja utakosa migogoro isiyokwisha kama
viongozi hawawezi kuelewana na kupanga mambo yakapangika timu haiwezi kwenda na
mtaishia kufungwa kila siku kwani uongozi wa vilabu hivi hauna tofauti na
vijiwe vya kuvutia Mihadarati wakati mwingine fujo na maelewano yasiyokwisha
makundi yanayotaka na yasiyotaka Baadhi ya viongozi wenye misimamo tofauti.
Mishahara ya makocha
hapa unaweza kulimbikiziwa mishahara yako mingi na unaweza kujiuliza hawa pesa
zao huwa wanapeleka wapi na kila siku unaskia vilabu hivi uongozwa na matajiri je
matajiri hawa wanafanya biashara gani ukiacha hayo yooote unafikiri kwanini
simba na yanga mpaka leo zimeshindwa kufanya Vizuri mashindano ya kimataifa hii
yote ni kwasababu ya kubadilisha makocha kama shati .
Siku zote huwa nasema
kuwa ili tufanikiwe katika soka yetu jambo la kwanza vilabu vya Tanzania
vinatakiwa kubadili utaratibu wa kiuendeshaji tofauti na uliopo sasa Rais wa
tff Jamali Malinzi huwa anasema kuwa
atanaka kutengeneza timu ya taifa ya chini nya miaka kumi na tano kwa maana ya
Under 12 ilikifika miaka kumi na saba tushiriki michuano ya afrika kwa sasa
nionacho ni kazi bure Tanzania haiitaji hayo
kwa sasa Shirikisho linahitaji kuunda utaratibu wa kuvisimamia vilabu
vinavyoongozwa na kuendeshwa kwa kutumuia wanachama ,kusimamia miundo mbinu ya
kisoka ,Elimu ya soka kwa wachezaji ,vilabu ambavyo vinaendeshwa kwa mfumo wa
hisa wa kampuni haina haja ya kuvisimamia kwa sababu zinajiendeshea kimpango
wake .
Ukiwa kama kocha
kabla hujakwenda kwenye nchi husika lazima ujue tabia ya wachezaji
,Viongozi,Mashabiki wanchi unayokwenda Sidhani kama hawa makocha wanafanya
utafiti wangekuwa wanafanya utafiti wasingekuwa wanakuja kufundisha Tanzania
kwa sababu ya utaratibu mmmbovu wa kiutawala na miundo mbinu.
Kwa sasa Tanzania
kuna makocha watano wa Kigeni lakini hakuna hata kocha hata mmoja wa Tanzania
ambaye anafundisha Nchi moja ya Afrika mashariki na kati je unafikiri ni
kwanini ?
Hapa tunaweza sema
kuwa hatuna makocha wenye Elimu ya kufundisha au ndio tuseme kuwa Tanzania tunalazimisha
mchezo tulioshindwa kucheza na kama tumeshindwa tufanye nini?
Shida moja kubwa ni
kuwa kila kiuongozi wa soka anataka afanye mabadiliko kwa hatua kubwa hata kama
hana muda wa kufanya hivyo kwa sasa soka ya Tanzania inavyofanya ni kama mtu
anayejaribu kwenda Sherehe akiwa amevali suti huku kaoga Passport size, kapiga
mswaki lakini hajachana nywele,hajavaa tai rangi ya koti na salawili tofauti
kashika simu lakini haina salio la kutosha anapanda piki piki ambayo
mwendeshaji hana Leseni huku element wote wakiwa hawana boda boda haina mafuta
na sheli ni mbali kwa utaratibu huu hata Sudan ya kusini ,Somalia,Eritrea
zikitulia na kuacha kipigana zitatupita.
Ni dhahiri
hatujielewi kwa hiyo nisingeweza kuja kufundisha soka Tanzania Nchi ambayo hata
Vyombo vya habari vinachangia kuharibu soka lake kwani vinapenda kukuza
migogoro isiyokuwa na msingi kuandika habari kishabiki kujaza wachezaji sifa ambazo hawana kwani
mfumo huuu Tanzania haita weza kufanikiwa kisoka mpaka Yesu au nabii Isah
atakaporea Tena.
Hizi ndizo sababu
ambazo zingenifanya nisje kufundisha soka Tanzania.
No comments:
Post a Comment