Klabu ya soka ya Yanga leo imetoka suluhu bila kufunga (0-0 )
dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar ya Manugu mkoani Morogoro katika mchezo uiofanyika katika dimba la Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Young Africans ikicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu kwa
takribani wiki mbili baada ya kutolewa katika mashindano ya kimataifa
iliwakosa wachezaji wake wanne mlinda mlango Deo Munish "Dida" ambaye ni
majeruhi, Mbuyu Twite (ruhusa), Haruna Niyonzima (malaria) na Mrisho
Ngasa (majeruhi).
Katika mechi ya leo mjini Morogoro, mchezo
ulikosa radha kwa timu zote kutokana na mvua kubwa zilizoyesha mjini
Morogoro na kusababisha wachezaji kushindwa kuonyesha ufundi wao na
kujikuta mara nyingi wakiteleza na kukosa mipira au mipira kuwapita na
kutoka nje.
Washambuliaji wa Young Africans walifanya mashambulizi
kadhaa langoni mwa Mtibwa Sugar kupitia kwa washambuliaji wake Emmanuel
Okwi, Didier Kavumbagu, Saimon Msuva na Hamis Kizza lakini walikuta
mipira yao ikiokolewa na walinzi wa Mtibwa Sugar na mingine kutoka meta
kadhaa pembeni ya lango.
Dakika ya
82, 84, 87, 89 na 90 Young Africans ilikosa nafasi za wazi za kuweza
kujipatia bao kupitia washambuliaji wake Okwi, Didier na Javu baada ya
mipira waliyoipiga kuokolewa na golikipa Sharrif Husein na mwingine kugonga
mwamba na kutoka nje na kona ambazo hazikuzaa matunda.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Mtibwa Sugar 0 - 0 Young Africans.
Aidha kwa upande wa Mtibwa mchezaji Abdallah Juma alizawadiwa kadi nyekundu kwa kosa ambalo bado halikuoneka kirahisi
AZAMA COMPLEX
Azam fc 4-0Coast union
AZAMA COMPLEX
Azam fc 4-0Coast union
No comments:
Post a Comment