Klabu ya Simba itafanya mkutano wa
wanachama wake Jumapili (Machi 16 mwaka huu) kwa ajili ya kuifanyia marekebisho
Katiba yao.
Nachukua fursa hii kuwatakia kila la
kheri katika mkutano huo ambao ni muhimu katika kuhakikisha klabu yao inapiga
hatua katika maendeleo ya mpira wa miguu na ustawi wake kwa ujumla.
Hata hivyo, nawakumbusha viongozi na
wanachama wa klabu ya Simba kuwa marekebisho hayo ni lazima yafanyike kwa
kuzingatia Katiba, Kanuni na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), Afrika (CAF) na Tanzania (TFF).
Aidha waraka wa TFF kwa wanachama wake
wa Februari 7 mwaka huu uzingatiwe kikamilifu katika marekebisho hayo.
TFF inawatakia wanachama wa Simba
mkutano mwema, na inawakumbusha wazingatie umuhimu wa kudumisha amani na
maelewano katika klabu yao.
No comments:
Post a Comment