Semina ya siku mbili kwa waamuzi wenye beji za
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu nchini
(elite) kwa robo ya kwanza ya mwaka huu inaanza kesho (Machi 15 mwaka huu)
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi na waamuzi wasaidizi 22 kutoka Tanzania
Bara na Zanzibar wanashiriki katika semina hiyo ambayo pia itahusisha mtihani
wa utimamu wa mwili (physical fitness test), na itamalizika keshokutwa (Machi
16 mwaka huu).
SIKIZA HAPA
Baadhi ya waamuzi hao ni Charles Simon kutoka
Dodoma, Dalila Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu
(Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam),
Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama (Iringa) na Jesse Erasmo (Morogoro).
John Kanyenye (Mbeya), Jonesia Rukyaa (Bukoba),
Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya
(Morogoro), Mfaume Nassoro (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame
(Zanzibar), Ngaza Kinduli (Zanzibar), Ramadhan Ibada (Zanzibar) na Waziri Sheha
(Zanzibar).
YANGA KUIVAA MTIBWA SUGAR VPL
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea
kesho (Machi 15 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo mabingwa watetezi Yanga
wataumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Nao vinara wa ligi hiyo, Azam
wanaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayofanyika Uwanja wa
Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mechi nyingine itachezwa Uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba kwa kuwakutanisha wenyeji Kagera Sugar dhidi ya maafande
wa Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya.
WATANZANIA WATANO WAKWAA UKAMISHNA CAF
Watanzania watano wameteuliwa kuingia
kwenye jopo la makamishna watakaosimamia mechi mbalimbali za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa mwaka 2014 hadi 2016.
Kwa mujibu wa orodha iliyotumwa na CAF
kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Watanzania hao ni Alfred Kishongole
Rwiza wa Mwanza na Hafidh Ali Tahir wa Zanzibar ambao wamerejeshwa tena kwenye
jopo hilo.
Rwiza na Tahir ambao ni waamuzi wastaafu
wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wakufunzi wa uamuzi walikuwepo
kwenye jopo lililopita la 2012 hadi 2014.
Makamishna wapya kwa upande wa wanawake
ni Elizabeth Mwanguku Kalinga wa Mbeya na Isabellah Hussein Kapera wa Dar es
Salaam. Kamishna mwingine mpya kwa upande wa wanaume ni Muhsin Ali Rajab kutoka
Zanzibar.
Wakati huo huo, CAF imeandaa semina kwa
makamishna wanaume itakayofanyika jijini Cairo, Misri kuanzia Aprili 3 hadi 4
mwaka huu.
Watoa mada kwenye semina hiyo ya siku
mbili ni Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani, Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF,
Shereen Arafa na Naibu Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF, Khaled Nassar.
Wengine ni Meneja wa Waamuzi wa CAF, Eddy
Maillet, Mkurugenzi wa Habari wa CAF, Junior Binyam, Mkurugenzi wa Teknolojia
ya Mawasiliano wa CAF, Tarek el Deeb na Mkurugenzi wa Masoko na Televisheni wa
CAF, Amr Shaheen.
No comments:
Post a Comment