Bira shaka mpenzi msomaji utakabaliana nami kuwa katika wilaya zote za Dar es salaam ni wilaya mbili zenye viwanja vya maana vya kandanda vya soka katika Mkoa wa Dar es salaaam Nazo ni Temeke pamoja na Ilala lakini wilaya ya kindondoni hakuna kitu na nisifuri kwa upande mwingine. je hii ina maana gani na unaweza kuuliza kuwa inawezekanaje katika wilaya hii hakuna kiwanja cha maana cha soka au cha mchezo wowote ule .
Haya tutazame je ni kweli hakuna kiwanja cha michezo jibu ni vipo lakini havipo ! ndio vipo lakini havipo najua unashangaa sababu kubwa ni kwamba viwanja vimeuzwa na havitumiki tena vipo kwa shughuri nyingine Binafsi lazima watu waelewe kuwa viwanja vivyopo sasa vimeshikwa na watu ambao hawana mapenzi mema na michezo kwa taifa la Tanzania mfano mdogo na hai ni huu kiwanja kilicho wazi cha Tanganyika Packers ambacho zamani kilikuwa kikitumika kwa kuzalisha nyama ya Ng'ombe sasa hakipo tena na yamebaki magofu tu jee nini kinaendelea katika kiwanda na uwanja ? ni kwa zaidi ya miaka ishirini sasa eneo hilo lipo hivyo hivyo na hakuna mwendelezo wowote .
Je nini kinaweza kukikumba kiwanja hicho ni kuvamiwa na fisadi na kuanza kubadilishwa na kujenga Supermarket ya kisasa kuhudumia watu ambao hawana pesa maishani mwao hivi tunajenga au tunabomoa ?
kwa miaka kumi ijayo hatutaweza kuwa na viwanja vya wazi na huo ndio utakuwa mwisho wa soka la Tanzania kwani viwanja vilivyopo sasa havina uhifadhi wa kuhudumu na kuna uwezekano mkubwa vikapotea kabisa hivi wizara ya michezo inafanya kazi gani katika mpango wa kuhakikisha viwanja hivi vinahifadhiwa na sio kuhifadhiwa na kuboreshwa katika hali ya juu ilituweze kupata ubora wa kimataifa na kuleta maendeleo lakini kwa sasa ni ndoto kwa sababu hakuna mpango mkakati wa kuhifadhi viwanja wazi na leo hii hata fukwe za Bahari kwa muda huu zimekwishauzwa je tutafika kwa mfumo huu ?
No comments:
Post a Comment