Tanzania ni nchi ambayo imetokea kuenzi viongozi wake kwa kuwapatia sehemu mbalimbali ili majina yao yatume katika viwanja au Barabara kama ukumbusho lakini siyo viongozi wote walio pata bahati ya kupewa heshima hiyo japokuwa wamelifanyia taifa mambo makubwa hasa wakati wa uhuru na kabla ya uhuru na baada ya uhuru lakini nia yangu sio kutaka kukuonyesha viongozi ambao hawajapewa heshima .
Wengi wetu tunamjua au kumsikia Edward Molinge sokoine aliyekuwa waziri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Aliyezaliwa mwaka (1 August 1938 – Kuawa kwa ajari Tar 12 April 1984) ni moja kati ya Viongozi waliopata heshima katika Jamhuri kwa ustadi mkubwa wa kazi zao yako mengi ambayo yamefanywa na kiongozi huyu lakini kuna kiwanja kimoja kipo mkoani mbeya ambacho kilijengwa na Manispaa ya Mji huo na kukipatia jina Waziri huyo .
Lakini sidhani kama sifa ya sokine inalingana na uwanja husika uwanja ambao siku ya mechi katika mbeya city dhidi ya Azam ikichezwa ilikuwa ikinyesha mvua ya hari ya kiwanja haikuwa ya kuvutia hata kidogo sehemu ya kuchezea haikuwa katika ubora uliohitajika mpaka leo bado haijafamika rasmi kwa idadi ya watu wanaoweza kuketi katika uwanja huo ,hakuna viti katika uwanja huo,hakuna taa jambo linaloashiria kuwa huwezi kucheza mechi wakati wa usiku uwanja huu uliwahi kuwekwa katika Orodha ya viwanja vinavyohitaji marekebisho na shirikisho la soka Tanzania tff .
Zipo huduma muhimu kama za choo ,na nyinginezo ambazo katika uwanja wa sokoine ni nadra sana kuviona katika ubora unaotakiwa je unadhani ni kosa la nani ?
ili kuuweka katika hari iliyo je kweli mzee Moringe angekuwapo uwanja ule ungekuwa katika hari ile au ndio Dharau na Dhihaka au ndio tunaendeleza sera za kuwapaka mafuta kwa mgongo wa Chupa kwa sababu kwa nchi yetu tumekuwa na kawaida ya kunukuuu kauli mbalimbali za viongozi kwa kazi zao ukiutazama uwanja wa sokoine na jina la Sokoine kweli tunamfanyia Dhihaka na matusi ya hari juu ipo haja ya kutazama upya sera za matunzo ya viwanja vyetu kwani sio tu kufanyiwa marekebisho bari havifai kabisa serikali na wadau tunatakiwa kutazama upya jambo hili.
No comments:
Post a Comment