Algeria imeunga na Nigeria katika hatua ya kumi na sita katika michuano ya Kombe la Dunia mara baada ya kutoka Sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Urusi katika mchezo wa Kundi H Urusi ndio waliokuwa wakwanza kupata goli lilofungwa na Kokorin katika dakika ya sita akiunganisha mpira wa krosi wingi ya kushoto na kumwacha mlinda mlango wa Algeria Rais mdomo wazi lakini Dakika ya sitini na sita SLIMANI alisawazisha goli akiunganisha mpira wa kichwa baada ya kupingwa mpira wa Adhabu Dogo upande wa kulia mwa Lango la Urusi .
Algeria inaifanya bara la afrika kuingiaza timu mbili kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la Duania mara kadhaa timu za afrika zimekuwa zikiingia raundi ya mtoano ambapo ni timu mmoja tu ambapo hufanikiwa kuingia hadi robo fainali .
katika hatua inafuata Algeria itapambana na Ujerumani ambapo mwaka 1982 Algeria ndio ilikuwa timu ya kwanza kuifunga ujerumani katika michuano ya kombe la Dunia .
Mchezo huo utachezwa siku ya jumatatu ambapo siku hiyo hiyo wawakilishi wengine kutoka afrika Nigeria itakumbana na Mabingwa Dunia mwaka 1998 ufaransa timu nyingine za afrika zilizo fungasha virago ni ghana ambao wametandikwa mbili sifuri dhidi ya ureno wakati ivory wakitandikwa mbili sifuri dhidi Ugiriki
wakati Cameroun wakichapwa nne sifuri na wafalme wa samba duniani Brazil
Matokeo mengine ya timu za Afrika hayako sawa kaka, umetupotosha au umepotosha wasioangalia mechi husika.
ReplyDelete