Angel Di Maria's amefunga Goli katika dakika za Nyongeza na kuipeleka Argentina katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea Nchini Brazil na huku ikicheza mpira ambao haukuvutia sana katika mchezo huo wa kumi na sita fanali Dhidi ya Switzerland.
Mabingwa hao mara mbili waliumiliki mchezo huo kwa kiasi kikubwa , Lakini walishindwa kufunga goli katika dakika za kawaida Hadi pale Di Maria alipounganisha pasi kwa ustadi kutoka kwa
Lionel Messi's .
Mlinzi wa Switzerland Blerim Dzemali alipiga mpira wa kichwa uliokwenda kugonga mlingoti wa Goli la Argentina Baada ya Di Maria's kufunga goli la ushindi .
Argentina sasa itakumbana na Belgium au USA katika Robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia jumamosi.
No comments:
Post a Comment