Algeria imeienyesha ujerumani licha kufungwa mabao mawili kwa moja katika muda wa Nyongeza ambapo mabingwa mara tatu ujerumani sasa wanaingia kwa mara ya tisa mfululizo katika hatua ya Robo fainali .
Vijana kutoka Afrika ya Kaskazini waliwakalia koo wajerumani lakini katika dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza muda wa Nyongeza
Andre Schurrle's aliuparaza mpira akiunganisha pasi aliyopatiwa na Thomas Muller's na Kijana kutoka Arsenal Mesut
Ozil's alifunga Goli la pili na kuhihakikishia Ujerumani nafasi ya kwenda Robo fainali .
Algeria ilipata goli katika Dakika za mwisho Goli ambalo liliipa faraja tu vijana hao kutoka afrika ya kaskazini Goli lililofungwa na Abdelmoumene Djabou.
Ujerumani sasa itakumbana na Mabingwa wa Dunia Mwaka 1998 Ufaransa siku ya Ijumaa huko Rio de Janeiro .
No comments:
Post a Comment