MaGoli yaliyofungwa na Kevin De Bruyne na Romelu Lukaku katika Dakika thelathini za Ziada yameiwezesha kuisukuma nje timu ya taifa ya Marekani na kuivusha Ubelgiji katika hatua ya kumi na sita bora na kuingia robo fainali katika mashindano ya Kombe la Dunia .
Mlinda mlango Tim Howard alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo mikali na kuisadia timu ya kwenda mpaka muda wa Nyongeza na Baadaye kufungwa na De Bruyne kwa shuti dogo la chini chini .
Lukaku's alifunga bao la pili liloonekana kama limemaliza mchezo lakini kijana Julian Green alirejesha goli moja kwa mpira maridadi akiunganisha juu kwa juu .
lakini ubelgiji walijitahidi kulinda magoli yao ya uongozi licha marekani kulihemea Lango ubelgiji kwa Muda wote uliobaki na sasa watapambana na Argentina siku ya Jumamosi .
No comments:
Post a Comment