Germany imefuzu katika hatua ya Nusu fainali na kuweka Rekodi ya kufika katika hatua hiyo kwa mara nne mfululizo ambapo goli la Mats Hummels' katika kipindi cha kwanza lilitosha kabisa kuibamiza ufaransa
Mlinzi Hummels alimzidi akili Raphael Varane na kupiga kichwa mpira baada mpira wa adhabu ndogo kutoka kwa Toni Kroos's .
Mlinda mlango Manuel Neuer alizuia michomo ya Mathieu Valbuena's kabla ya Karim Benzema's kupiga na kuzuiliwa na mlinda mlango huyo .
MGermany' Andre Schurrle alipga mpira mwepesi ambao Hugo Lloris aliokoa kabla ya Neuer kukokoa kwa kiganja cha mkono shuti la Benzema's na kujihakikishia ushindi kwa ujerumani.
Joachim Low's na timu yake sasa watapambana na mshindi kati ya Brazil na colombia ili mmoja akacheze fainali .
No comments:
Post a Comment