Timu ya soka ya Taifa ya Brazil's Imemaliza michuano ya kombe la Dunia vibaya mara baada ya kubamizwa mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya uholanzi .
Robin van Persie alifunga goli la kwanza kwa mkwaju wa penati mara baada ya Roben kuangushwa na Thiago silva katika Eneo la hatari .
Daley Blind aliongeza matatizo kwa Brazil baada ya kufunga bao la pili wakati David luiz alipookoa mpira Vibaya na kukumkuta Mfungaji.
Brazil ilionekana kurejea mchezoni lakini mambo yalizidi kwenda vibaya katika dakika za mwisho Georginio Wijnaldum aliunganisha klosi toka wingi ya kulia na kufunga bao la tatu na kuhitimisha kabisa ndoto za brazil kutamba katika michuano ya Kombe la Dunia .
No comments:
Post a Comment