Baada ya tuhuma zakumdunda meneja wake, hatimaye bondia wa ngumi za
kulipwa anayeshikilia mkanda wa WBF, Francis Cheka, amepandishwa
kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, akikabiliwa
na shtaka la shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi.
Cheka amefikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu
mkazi mkoa wa Morogoro, na kusomewa shtaka, na mwendesha mashtaka wa
polisi, Aminata Mazengo, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Said Msuya,
akidaiwa mnamo julai 02 mwaka huu, bila halali na akijua kufanya hivyo
ni kosa kisheria, amempiga kwa ngumi maeneo ya kichwani na tumboni,
Bahati Kabanda maarufu kama Masika, na kumsababishia maumivu makali.
Cheka anadaiwa kutenda kosa hilo kwa kabanda ambaye alikuwa ni
meneja wa baa yake ya Vijana Social iliyopo sabasaba katika manispaa ya
Morogoro baada ya kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu ya mauzo, ambapo
mahakama ilitoa masharti ya dhamana, ikimtaka kuwa na wadhamini wawili
kwa kila mmoja kuweka dhamana ya maandishi ya shilingi milioni moja, ama
aende rumande, ambapo hadi ITV inaondoka mahakamani hapo, taratibu za
dhamana zilikuwa zikiendelea.
ACKNOWLEDGE ITV
No comments:
Post a Comment