Kocha Mkuu wa Timu ya soka ya Taifa
ya Tanzania Mart Noij amesema timu yake itacheza kwa umoja ilikuhakikisha
inapata ushindi katika Mchezo wa kutafuta Timu
itakayoingia kucheza kwenye Makundi ambayo yatatumika kufuzu fainaliza Kombe la
Mataifa ya afrika huko Morocco ambapo stars itakuwa inakipiga Dhidi ya Msumbiji
siku ya jumapili katika uwanja wa taifa jiji Dar Es Salaam.
SIKILIZIA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI
WA HABARI
Kikosi cha Stars, ambacho kilikuwa Kambini huko Botswana kwa Wiki
mbili na kisha kwenda Mbeya, kimeimarika kwa kuwapata Maprofeshenali
wake Watatu ambao ni Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wa Klabu ya TP
Mazembe ya Congo DR na Mwinyi Kazimoto anaechezea Klabu ya Al Markhiya
ya Qatar.
Kwenye Raundi iliyopita, Taifa Stars iliibwaga Zimbabwe kwa Jumla ya
Mabao 3-2 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza Bao 1-0 Jijini Dar es Salaam
na kutoka 2-2 huko Harare.
Mshindi wa Mechi kati ya Taifa Stars na Msumbiji ataingia Kundi F ambalo lina Timu za Zambia, Cape Verde na Niger.
No comments:
Post a Comment