Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya riadha inayoondoka
kesho Julai 16, 2014 kwenda Glasgow, Scotland, kwenye Michezo ya Jumuiya
ya Madola kwenye hafla fupi ya kukabidhi bendera iliyofanyika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernand Membe, Naibu Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Juma Nkamia na wadau wa michezo.
Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzanai Jakaya Mrisho
Kikwete hii leo amekutana na wachezaji wa timu ya taifa ambao watakwenda mjini
Glasgow nchini Scotland kushitriki michuano ya jumuia ya Madola ambayo
imepangwa kuanza July 23-August 03 mwaka huu.
Raisi kikwete amekutana na wachezaji hao jijini Dar es
salaam na kuwahusia suala la kujituma wakati watakapokuwa kwenye michuano hiyo
ambayo hushirikisha nchi mbali mbali duniani kote.
Kikwete amewataka wachezaji wa Tanzania kutambua thamani
waliyopewa ya kwenda kuiwakisha nchi kwenye michuano hiyo, hivyo amewasisitiza
suala la kutambua umuhimu wa kiu ya mashabiki pamoja na wadau wa michezo
nchinia mbao kwa miaka mingi iliyopita wamekua na hamu ya kuona angalau ushindi
wa medali moja ya dhahabu unapatikana.
Naye katibu mkuu wa kamati ya Olympic Tanzania Filbert Bayi
ameishukuru serikali ya aawamu ya nne kwa mchango mkubwa iloiyoutoa kwa mwaka
huu katika maandalizi ya timu ya taifa kwa kukamilisha mpango wa kambi ya nje
ya nchi.
Bayi amesema anaamini huo ni mwanzo ambao unatoa mwanga kwa
taifa la Tanzania ambalo lina hamu ya kurejesha heshima yake katika Nyanja ya michezo
duniani.
No comments:
Post a Comment