Argentina itapambana uso kwa uso na Ujerumani katika fainali ya kombe la Dunia siku ya jumapili baada ya kuifunga Uholanzi kwa mikwaju ya penati katika jiji la Sao Paulo.
Nafasi kadhaa zilipatikana katika muda wote wa dakika mia moja na ishirini ,
Argentina's kupitia kwa Gonzalo Higuain alipata nafasi nzuri lakini alipiga mpira uliokwenda nje ya lango na kugusa nyavu za nje katika muda wa kawaida.
Sergio Romero alipiga shuti liliokolewa na beki wa uholanzi Ron Vlaar na Wesley Sneijder walikosa penati na baadaye Maxi Rodriguez kufunga .
Penati yake inaipeleka Argentina katika mchezo wa fainali utakaochezwa jumapili katika uwanja wa Maracana na hii inakuwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 90 ambapo timu hizi zilikutana na ujerumani kutwaa kikombe 1990.
No comments:
Post a Comment