Manchester City imeendeleza Rekodi ya Asilimia mia moja ya kuanza vizuri katika Ligi kuu ya Uingereza katika harakati zao za Kutetea Ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza kwa Kuifunga Liverpool bao tatu kwa moja .
City ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango Mara Baada ya Stevan Jovetic kufunga akitumia mwanya wa walinzi wa Liverpool kuokoa mpira vibaya kutoka kwa mchezaji aliyecheza kwa mara ya Kwanza Alberto Moreno na kuumpa nafasi ya kumfunga Simon Mignolet.
Jovetic alifunga bao la pili ,akipokea pasi iliyorejeshwa Nyuma na Samir Nasri's , na baadaye Sergio Aguero akitokea kwenye Benchi alifunga bao la Tatu akipokea pasi kutoka kwa Jesus Navas's.
Majogoo hao wa Anfield walikuwa wageni wa Man city , Huku mchezaji waliye mnunua kwa Dau la Pauni milioni £16m Mario Balotelli akiutazama mpira huo katika majukwaa ya watazamaji , Liverpool ilirejesha goli moja baada ya Pablo Zabaleta's kujifunga dakika za mwisho wa Mchezo .
Man city 3-1Liverpool
No comments:
Post a Comment