Mpenzi msomaji Mwisho wa Juma hili nilikuwa katika uwanja wa Taifa mara ya mwisho kukanyaga uwanja huu ilikuwa mechi baina ya Tanzania Dhidi ya Algeria kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia .
Tangia siku hiyo sikukanyaga Tena uwanja wa Taifa mpaka nilipofika Jumamosi Tar 23 siku ambayo Real madrid ilileta Magwiji kuja kupambana na Mastaa wa Tanzania .
Zipo sehemu nyingi za kukaa kwenye uwanja ule japokuwa waandishi wa habari bado hawajatengewewa sehemu maalum ya kukaa kwa Bahati Nzuri nilikaa upande ambao unaaminika ni wa Yanga na nilikaa mbele upande wa kushoto ,na Kushoto kwangu kwa maana ya jukwaa kuu alikuwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati Chini ya yake walikaa watu ambao ukiwatazama unaweza kuwadharau lakini walikuwa ni watu wa protoco sio rahisi Mashabiki wa kawaida kukaa Eneo hili pindi Rais awapo kiwanjani Tuachane na Hilo .
Moja kati ya Picha ambazo nilizipiga ni Hiii unayoina ya Hapo kocha Mkuu wa Timu ya Soka ya taifa ya Tanzania taifa Stars Mart Noij Ignatius Ukiitazama picha hii inakupata Habari Nyingi Kichwani Mwake pengine haya ndio aliyokuwa anawaza kwenye Ubongo wake!!
Hawa wa Tanzania wanapenda Mpira lakini Tatizo wanataka maendeleo ya Haraka !
Hivi hawa Tanzania 11 walishindwaje kufanikiwa mbona kama wanauwezo kuliko Taifa stars?
Lakini hawa mashabiki wanapenda kuwaona mastaa wa ulaya kuliko wa Kibongo?
Wanakiwanja kizuri lakini hakuna jambo lolote wanaloweza katika soka !
Je unafikiri ni swali lipi ambalo linaweza kupata jibu la Haraka ukitazama picha sidhani kama anaweza kupata jibu la haraka hata kidogo kiukweli soka ya Tanzania limeshindikanika katika vilabu vya soka Vya Tanzania na labda sasa litegemee watu kama akina kipingu ambao kwa mapenzi yao binafsi soka ndio wanatengeneza wachezaji ukitazama katika miaka ya Elfu Mbili Makongo ndio waliokuwa wakiongoza kwa kutoa wachezaji wengi kwenye timu za Tanzania Nadhani Noij yalikuwa ni moja kati ya Mambo aliyokuwa akiyawaza na Bila kupata Majibu ya Msingi kwasasa Tanzania kilichobaki ni Kushekherekea ujio wa Mastaa kuja Tanzania, lakini sio kufanya Jitihada za kutafuta nafasi za kupeleka wachezaji ulaya ningekuwa mimi ningeomba watusaidie kutengeneza wachezaji Real madrid .
Lakini kocha tuliye naye ni Mholanzi tunashindwaje kumuomba atusaidie kuomba urafiki na Ajax lakini wapi tumelalala utafikiri Pono Bahari .
Tumekuwa Mahodari tu wa Kusema na Kuimba Oooooh Oooh Tanzania
kutenda Sifuri Haya Naishia hapo.
No comments:
Post a Comment