Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anatarajia kufungua Kozi
ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) inayoanza kesho (Agosti 6 mwaka huu) Msimbazi Center jijini Dar
es Salaam.
Kozi
hiyo itakayokuwa na washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka
huu na itaendeshwa na Wakufunzi kutoka FIFA na itafunguliwa saa 3
asubuhi. Wakufunzi hao ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau
(Tanzania) na Senka Kanyenvu (Botswana).
Baadhi
ya washiriki wa kozi hiyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman
Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah,
Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
Wengine
ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud
Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal
Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu
wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona),
Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama),
Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa
Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement
Sanga.
Washiriki
wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi,
Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na
Matukio, Jimmy Kabwe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba.
Wengine
ni Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa
Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na
nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
No comments:
Post a Comment