Diego Costa amefunga magoli mawili huku Chelsea ikipata ushindi wa Kushangaza katika Dimba la
Everton Wakiilinda Takwimu yao ya Asimilimia 100% ya ushindi katika msimu mpya Ligi kuu ya Uingereza .
Everton walijitahidi kurejesha magoli yao kutoka goli mbili nyuma lakini jitihada zao hazikuweza kufua dafu sana mara baada ya kujikuta katika Dakika kumi za Mwisho wakiruhu mabao matatu.
Lakini Jose Mourinho's aliweza kuhimili mikimiki ya mechi hiyo nakuondoka na alama tatu muhimu huku wakionyesha uwezo tofauti na ule wa mwaka jana baada ya kufungwa 1-0 msimu uliopita katika Dimba la Goodison Park muda kama huu mwaka jana .
Tangia hapo , Magoli yalikuwa yakiingia kwa upande wa Chelsea baada ya wapinzani kuzidiwa katika sehemu ya katikati ,Kitu ambacho hakuna ambaye angeweza kuwalaumu katika muda huu wa msimu .
Hata baada ya kumuondoa mchezaji aliyeigharimu £50m Fernando Torres wiki hii , Waliweza kuonyesha namna gani walivyoweza kusajiri msimu huu na kuonyesha mabadiliko makubwa -Hasa pale safu ya Ulinzi ya Everton ilivyoonyesha Udhaifu Mkubwa katika kuzuia mashambulizi .
Costa alihihakikishia ushindi timu yake huku akinonyesha kuwa kiwango kilichotumika kumnunulia kilikuwa sahihi £32m akitokea Atletico Madrid baada ya kufunga goli katika Sekunde ya 35 , akikimbia kwa kasi huku akiisubiri pasi kutoka mchezaji mwenzake mpya , Cesc Fabregas.
MATOKEO MAKUBWA KUTOKEA EPL |
---|
No comments:
Post a Comment