Wengi tulivyokuwa hatuna aibu hata ya kushngaa tutaanza kumsifia mchezaji mpya wa Daraja la Chini kule Brazil Genilson Santana Santos ‘Jaja’ ambae leo amejichotea sita za bure mbele ya kocha Mbrazil,
Marcio Maximo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 kwenye
mechi ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Binafsi nimemtazama mara kadhaa katika mazoezi ya yanga paleLoyola la msingi ni kuwa Kocha Marcio maximo Tangu akiwa katika timu ya taifa ya Tanzania leo amewatukana Rasmi watanzania tena kisomi kwa kuwaeleza kuwa Hatuna mshambuliaji .
Binafsi ukimtazama Jaja ni mchezaji mbaye ana umbo kubwa mwenye mwili mzito kidogo lakini mwingi wa akili ukitazama goli la kwanza na la pili jaja amezoea kufunga tangu akiwa kwao Brazil .
Marcio alivyokuwa Timu ya taifa ya Tanzania alikuwa mara kadhaa akitafuta washambuliaji na wamepita wengi lakini leo ameaumua kuwaeleza ukweli kuwa hakukuawa na mshambuliaji katika timu ya taifa ya Tanzania
Binafsi nimeanza kuiona yanga ambao sikuwa kuiona kabisa kwa miaka mingi fizikia ,umakini wa viungo uimara wa safu ya ulinzi wakati fulani tuwe tunashawishika kuangaalia Sayansi ya soka inakwendaje lakini sio kupiga zogo tu ohooo yanga ,yanga simba ,simba, Azam kiboko yao swala kubwa wachezaji na uwelewa kwa walimu nadhani leo marcio maximo katufundisha jinsi ya kuwa na mshambuliaji anayejua kufunga .
Si ajabu watu wataanza kukumbuka na kuanza kusema arejeshwe kwenye timu ya taifa ndio tulivyo sisi tuna ulimbukeni wa hali ya juu kweli ni kipi hasa tulichomwondolea Maximo leo anakuja kukifanya katika ardhi ya Tanzania tena kwenye timu yetu ya kizalendo sasa shida nini ?
Hatuna wafungaji magoli tunawabahatisha magoli kwa miaka miwili iliyopita mfungaji bora katika nchi nyingine kwenye ligi yetu hii ni aibu tosha
Leo kule kwenye magazeti ya Kireno Brazil watashangaa kuona kijana asiyejulikana katika fukwe za kopa capaba anaonekana Dhahabu hapa ndipo tunapoonyesha kiwango chetu cha juu cha ujinga tulinao ambao maximo katufundisha hakuna mafanikio ya Haraka katika soka .
|
14 September 2014
MAXIMO ANATUELEZA KUWA HATUNA MSHAMBULIAJI WA AINA HII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
lisungu_chisara@yahoo.com
TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA
No comments:
Post a Comment