Makamu wa rais FIFA Prince Ali Bin Al-Hussein ametoa fursa ya kuendelea kwa shirikisho hilo Kuzizawadia Nchi nyingine nafasi ya Kuandaa michuano ya Kombe la Dunia Nchi ambazo hazijawahi kundaa kombe Hilo japokuwa kulikuwa na Utata katika kuizawadia Qatar kuandaa michuano ya mwaka 2022 .
FIFA
imeipa Fursa ya kuandaa michuano ya 2018na 2022 kwa Nchi za Urusi na kama ilivyokuwa kwa 2010 kwa afrika kusini ,lakini kulikuwa na Taarifa zilizosema kulikuwa na vitendo vya Rushwa vilivyomhusisha Mohamed Bin
Hammam katika gazeti Sunday
Times ambazo zilimuangusha makamu huyo wa rais wa zamani wa fifa ambapo iliripotiwa kuwa alitoa rushwa kununua Baadhi ya Wapiga Kura kuipa nafasi
Qatar.
Kwa mujibu wa Mchunguzi wa Kanuni za uchunguzi za FIFA Michael Garcia aliwasilisha ripoti yake mwezi May na ,huku zikihusisha kuwa mashindano ya kombe la Duania hayatafanyika sehemu nyingine yoyote ile Zaidi ya Qatar 2022 , Prince Ali amesisistiza kuwa ni jambo la kawaida kwa nchi zinazotaka kuandaa kombe hilo kupata uzoefu ktoka kwa Qatar .
'Sikuwepo wakati wakipeleka maombi ya kuandaa mashindano hayo sasa siwezi kutoa maoni kuhusu yaliyotokea (kwa mwaka 2022). Nadhani kitu cha muhimu ni kuwa tutakuwa tuna makombe mawili ya Dunia tena mazuri zaidi.
'Ni jambo la muhimu kwa kombe hili likaandaliwa kila bara ili litembee Duniani kote ,mimi ni msimamo wangu kuwa litawezekana , Sasa inabidi tuwe na matumaini kuwa linaweza kufanyika kwa njia sahihi na kila kitu kinaweza kufanyika kwa ufanisi zaidi ili tufike mafanikio ,bila kujari yatakuja maamuzi gani .'
Prince
Ali,ambaye pia ni Rais wa Chama cha soka cha Jordan , alikuwa akizungumzia ujio wa kombe la dunia katika bara lake miaka nane ijayo ' -
Anasema : 'Ni jambo zuri kwa kila mmoja pale kombe la dunia linapoandaliwa katika bara lake . Nikisema hivo , Tunayofuraha kubwa sana kuandaa michuano ya kombe la dunia kwa Umri chini ya 17 kwa wanawake na kombe la dunia la mwaka 2016,Kwani nina furaha sana na kila kitu kitakuwa sawa .
No comments:
Post a Comment