HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

24 December 2008

Maradona vs Geoff hurst

UCHUNGU WA KUFUNGWA UNAPOKOSOA MAKOSA YA MWENZAKO ANGALIA BOLITI LA JICHO Habari za leo wapenzi wasomaji wanablog .leo katika makala yetu tutazungumzia uchungu wa kufungwa magoli yasio halali hasa pale unapocheza na hasimu wako wa jadi. wiki iliyopita kulikuwa na mechi za kimataifa zilikuwa nyingi ikiwemo mechi baina ya Tanzania na msumbiji na ulaya zilikuwa nyingi kati uingereza na ujerumani, argentina na uskochi. Lakini leo kitu ambacho nataka niwaambie kuwa hakuna watu wasiopenda kufungwa magoli yasio halali na mwamuzi kukubali kama uingereza lakini ndio wakwanza kusherekea magoli ya aina hiyo wanaposhinda wao, kabla ya mechi ya kirafiki baina ya Argentina na uskochi nilikuwa nikitazama runinga na kumtazama Diego maradona akieleza shutuma zinatolewa na kocha wa uskoch alex Mc leish wakimtuhumu Gwiji huyo kwa kufunga goli alilolipa jina la mkono wa Mungu waingereza husema Hand of god lakini maradona akajibu iweje leo mnanituhumu mbona ninyi mlishangilia goli ambalo alikuvuka mstali akizungumzia goli alilofunga Geoff Hurst pale wembley haya leo tuangalie nani aliadanganya kushinda mwenzie ukiangalila maradona katika picha ya mnato kweli alifunga na mkono na ni kweli mpira ulivuka mstari ukirudi kwa Geoff Hurst huyu akufunga kabisa goli kwani mpira aukuvuka mstari na likakubaliwa tena wakimfunga hasimu wao ujerumani katika fainali ya kombe la dunia mwaka 1966 na Mungu GEOF HURST AKIFUNGA GOLI AMBALO ALIKUFUVUKA MSTARI NA LIKAKUBALI DHIDI YA UJERUMANI KATIKA UWANJA WA TAIFA WA WEMBLEY NCHINI UINGREZA MWAKA 1966 KATIKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA NCHINI UINGEREZA. NAAM DIEGO ARMANDO MARADONA AKIFUNGA GOLI KWA MKONO AMBALO LIMETIZWA JINA LA THE HAND OF GOD KATAKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKA 1986 NCHINI MEXICO mkubwa aliwasahaulisha miaka ishirini hadi kufika mwaka 1986 kule mexico kwenye michuano ileile ya kombe la Dunia. kweli magoli haya yanauma mpaka inafika wakati watu wakasema kutoka vinywani mwao hatukusamei kabisa wakati biblia inasema samehe saba mara sabini pengine Mc Leish aliudhiwa zaidi na maradona kwani moja kati ya magoli ya kwanza ya kimataifa alifunga katika uwanja wa hampden park huko uskoch lakini leo wanapolaumu kuwa maradona ni muongo hivi angalia kati ya maradona na Geoff nani alidanganya au nani alifanya mchezo wa kimafia zaidi ya mwenzake ndipo unapo gundua kuwa mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu maana ukifungua website mbalimbali utaona maradona akiwa amevalia jezi ya taifa akinukuliwa akisema na apa na nukuu maneno hayo ya kiingereza “I don’t know why they blame me because even them they score the goal against Germany which didn’t cross the line “yani sijui kwanini wananilaumu mimi wakati hata wao walifunga goli ambalo alikuvuka mstari dhidi ya ujerumani. Kweli inauma sasa jenga picha katika ubongo wako kuwa hupo uwanja wa taifa halafu Simba na Yanga zinacheza halafu ni mechi ya mwisho ya ligi kuu dakika ya tisini timu moja wapo katika hizo inafungwa goli chagua mwenyewe lipi zuri kati ya la maradona na la Hurst je hali itakuwaje kiwanjani hiyo ni kukuonyesha uchungu wa magoli hayo lakini unaweza kuona timu ya taifa ya ujerumani hawazungumzii sana lile goli kwani wameshasahau au ndio Mungu anawatafutia sehemu mwafaka ya kulipiza kisasi kwakweli waingereza wamezidi kuongea sana waache kumlaani Maradona kwani soka ndivyo ilivyo . unapofanya fitina tena kama hizi tamu sana ukifanikiwa wewe lakini ukifanyiwa wewe na ukajua na dunia ikadhihirisha kuwa kweli aikutendeka haki yamkini huwa inauma sana kwa jamboa kama hili likikutokea ni fundisho hata hapa nyumbani pindi tufungwapo tunalalama ukiangalia kwenye mkanda wa video tofauti kabaisaa. Na zile lawama ambazo hutolewa na huo ndio utamu na uchungu wa magoli yasiyo halali.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers