HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

1 January 2009

michuano ya charenji cup

MICHUANO YA CHALENJI CUP Habari za leo wanablog kama kawaida leo tunaangalia timu ya taifa ambayo jumatano ya tarehe therathini na moja inakwea pipa kuelekea Kampala Uganda katika michuano ya chalenji cup michuano ambayo huzijumuisha timu za taifa za nchi mbalimbali katika ukanda wa afrika mashariki na kati ambapo bingwa mtetezi ni sudan nadhani unakumbuka wale tulio wakung`uta kwao bao mbili moja kule kwao na waka tupatia tiketi kiulaini ya kwenda cote d`voire timu yetu iliagwa jumatano na Mkuu wa mkoa wa dare s salaam Mh Abass Kandoro lakini kabla ya Mkuu wa mkoa kuzungumza alianza kuzungumza afisa Habari wa shirikisho la kandanda Tanzania TFF frorian rweimamu kaijage yeye alitoa utambulisha tu kwa waandishi wa Habari baadae akamruhusu Makamu wa pili wa rais wa shirikisho la kandanda la Tanzania Tff Ramadhani Nasibu iliamruhusu Mkuu wa mkoa wa dare s salaam azungumze. Athuman nyamlani makamu wa kwanza wa rais wa shirikisho la kandanda tanzania akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Abass kandoro. Nyamlani akachukua shavu naye akaanza kwa utani kwa kusema timu ya taifa ilipokuwa ikirejea kutoka Ougodougo Kule Burkinafaso baada ya kuingamiza wenyeji goli moja kwa bila likifungwa na Elasto nyoni mh alipanda loli bila kujizuia alijishtukia kafika holetelini kwa loli sasa akasema safari hii inawezekana mh Kandoro akapanda trekta kwa furaha ya ushindi naam akamkaribisha baba yetu wa mkoa azungumze. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Abass Kandoro akizungumza wakati akiiaga timu ya Kirimanjaro stars inyokwenda uganda kushiriki michuano ya charenji cup Naam mkuu wa mkoa alianza kwa kuwashukuru viongozi wote wa tff kwa kazi nzuri wanaifanya mpaka hivi sasa vilevile akatukumbuka nasisi tunaoandika Habari hasa wale spoti mkuu wa mkoa aliamua kukiri dhahiri furaha aliyonayo kusema kuwa timu ya taifa ya Tanzania ya leo sio ya miaka miwili iliyopita kwani alisema zamani timu ilikuwa ikienda kama washiriki lakini leo hii tunakenda kama washindani na akasisitiza kuwa mara nyingi tukienda kule huwatunakwenda na visingizio vingi vya maandalizi duni lakini leo hii tunakwnda tukiwa tujiandaa na kusisitiza ya kuwa raha tunayoipata sasa ni kwasababu timu yetu inatuunganisha kama taifa na akawambia ya kwamba endeleeni kwani mnailetea Tanzania heshima kubwa sana na akaongeza kuwa matunda haya ni uongozi mzuri wa tff na kocha mkuu Marcio maximo vilevile na wahisani na akawomba waendelee kuidhamini. Naam wachezaji mmefanya kazi kubwa sana kwani watu nchini kwa sasa wanawaanglia mtakapo kwenda cote d`voire kwaiyo tuta elekeza nguvu zetu zote Mashindano ya kampala yatumieni kama mazoezi ya kujiandaa kwenda cote d`voire acheni ubinafsi uwanjani mkuu wa mkoa akatia mkwara kuwa sisi ni tishio kwani anaamini hata Senegal wanatuogopa akaipa changamoto Tff kutuma watu wakaangalia mechi za wapinzani mwisho akawambia ninawatakiwa ushindi nendeni kwa matumaini na tutaendelea kuwa ombea lindeni heshima hasa za kwenu uwanjani kwani ni wakati muafaka kuonyesha ujuzi mlionao ili dunia na afrika iyelewe kwamba Tanzania ni tishio . Naam baada ya hapo shavu likawa la kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Marcio maximonaye akaanza”kabla ya yote naomba kutoa shukrani kwa sapoti mnayotuonyesha kwani ndicho kitu pekee kinachotupa nguvu na kutujengea stamina mda wote naongea na wachezaji wangu nilikuwa na Sunday kayuni na rais tenga na marcos tinoco kule coted`voire unajisikia vizuri kuona bendera ya Tanzania ya ikipepea katika ya mataifa kumi na sita bora barani afrika na inabidi tuelezea uharisia wa manbo harisi kwani Tanzania ndio kwanza tunaanaza kutembea na bado tunasafari ndefu kwa mfano sasa tuna mshindano ya chan lakini kabla ya hapo tunachalenji cup ambapo kuna timu kumi ni timu sita au tano ndio zinaweza kuchukua ubingwa na vilevli mnakocha ambaye anabadilisha timu hata kama inashinda tunakenda tukiwa na ujasiri lakini leo hii Tanzania tunakwenda kushindana na vilevile huwa hatutabili matokeo kwenye soka”. Hayo ndiyo yalikuwa mananeno ya Marcio maximo Kocha mkuu wa timu ya timu ya kirimanjaro marcio maximo akizungumza katika hotel ya Annex iliyopo Msasani jijini Dar es salaam Kocha mkuu wa kirimanjaro stara na taifa stars Marcio maximo akiwa na viongozi wa shirisho la kandanda tanzania na mkuu wa mkoa abass kandoro Baadae nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Henry Joseph naye akaongea kwa niaba ya wachezaji wa timu taifa tunashukuru kwa yote mliotufanyia nasi tutajitahidi kulinda heshima ya timu ya taifa na nchi kiujumla tunaahidi ushindi japokuwa leo sinamengi sana ya kuongea kwani tumejianda vyakutosha na tutajitahidi kwa uwezo wetu wote. Naam ulifika wa kati Mkuu wa mkoa kumkabidhi nahodha wa timu ya taifa ya tanzaina henry joseph naam tazama mambo yalivyo kuwa hapo chini Nahodha wa timu ya taifa ya tanzania Henry joseph akizungumza wa timu hiyo iliyokua ikiagwa kwenda uganda kwenye michuano ya chalenji cup Lakini kwajinsi nyingine timu ya taifa ya sasa ilikuwa imechanganyika na vijana watatu chini ya miaka kumi na saba kuonyesha jinsi gani inaweza kukomaza wachezaji iliwapate uzoefu wa kimataifa zaidi na kujenga timu ijayo . Naam hivyo ndivyo mabo yalivyokuwa hii siku hiyo ya kuagwa timu ya taifa. Moja kati ya wachezaji ambao waongezwa katika timu ya taifa ya wakubwa kutoka under seventeen Wachezaji wa timu ya taifa wakiwa wanamsikliza mkuu mkoa alipokuwa akiawaaga. Waandishi wa habari wakiwa wamejumuika na wachezaji wa timu taifa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika msasani Ramadhni nasibu makamua wa Rais wa shirikisho la kandanda akifuatilia jambo kwa umakini Nahodha wa timu ya Taifa ya tanzania henry joseph akipewa bendera ya taifa na mkuu wa mkoa wa dar es salaam abass kandoro Naam hapo chini katika picha tofauti unaweza kuona picha tofauti za wachezaji wakipeana mkono na mkuu wa mkoa wa dar es salaam JAMANI NINAWATEGEMEA HASA WEWEEE| MMH ANGALIA CHINI HAPO RAHA...............USIO HOFU KOMBE LAKWETU Hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa tunaiyakia kila la kheri timu yetu ifanikwe Mungu ibariki tanzania|

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers