HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 December 2012

FA KUCHUNGUZA AJARI YA FERDINAND


Chama cha soka cha Uingereza FA kimethibitisha kuwa kitaanza kufanya uchunguzi baada ya kutokea ajari ya kurushiwa kitu kisichofahamika kutoka Jukwaani  katika mchezo uliokutanisha timu mbili za mji mmoja yaani Manchester Derby ambacho kilimgonga  Rio Ferdinand. 

Ferdinand ameonekana kupigwa na Sarafu alipokuwa akishangilia bao la tatu dhidi man city, sasa swala hilo linashughurikiwa na maafisa polisi wakuuu wa jiji la Manchester na Maafisa wa FA 
Katika Taarifa iliyotolewa na FA Kuwa wanachunguza tukio hilo lililotokea baada ya goli la tatu  kufungwa ambapo   Rio Ferdinand
alipigwa na na kitu kinachodhaniwa kuwa ni sarafu


 FA italishughurikia swala hilo na kwa kushirikiana na maafisa polisi wa Manchester na wasimamaizi  wa majukwaa ambao walikuwepo wakati tukio linafanyika na waamuzi waliokuwa karibu na eneo hilo 


Msemaji wa  FA amesema : " ni jambo la kusikistisha hasa kwa ligi ya uingerza kutokea jambo kama hilo ambapo ulimwengu mzima unatazama .tuta lifanyia kazi swala hili  na klabu zote mbili ilikuweza kuwafahamu waliofanya kitendo hiki na adhabu kubwa kwa atakae patikana atafungiwa maisha kuto kuingia kiwanjani 


"Tunalaumu kitendo hiki na hakikubariki kwani kilimkata juu ya jicho na alipata matibabu  na kurejea kiwanjani  

"Mpira wa miguu nchi hii umeleta maendeleo makubwa katika miongo iliyopita tunatakiwa kuendeleza usalama na ulinzi ndani ya viwanja na watuhumiwa watapa adhabu kali  na kuwa fundisho kwa wengine 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers