HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

14 December 2012

Luzhniki Stadium NDIO KILA KITU KOMBE LA DUNIA 2018


Siku ya Tarehe  14 December 2012 , katika Mkutano wa mwisho wa mwaka huko   Tokyo,   kamati kuu ya Fifa imekipitisha kiwanja cha LUZHNIKI kuwa ndio kiwanja kitachotumika katika  mechi ya ufunguzi wa fainali za kombe la dunia na vilevile ndio kiwanja kitakachotumka kuchezea fainali ya kombe hilo la dunia , kiwanjani hicho cha kihistoria ni moja kati ya viwanja vichache vilivyopewa heshima ya kuaandaa mechi mbili kubwa katika mashindano makubwa kama hayo duniani.

Uwanja huu wa  Luzhniki ulifunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka  1956, umewahi kuaandaa matukio makubwa ikiwemo ufunguzi na ufungaji wa mashindano ya olympic   1980 ,na fainali za klabu bingwa barani ulaya mwaka   2008 .
Uwanja huo utafungwa mwezi  August 2013, kabla ya kufunguliwa tena miaka mitano baadae kupisha mataengenezo na kurekebisha muonekano wa kiwanja hicho hasa mwaka 2018.

Aidha katika fainali hizo kiwanja hicho pia kimepewa heshima nyingine ya kuandaa mchezo mmoja wa nusu fainali huku nusu fainali nyingine ikichezwa katika uwanja wa   St Petersburg.

Kiwanja cha  St Petersburg, ambacho kipo katika mataengenezo katika kisiwa cha Krestovsky , kitakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguizi na ya fainali ya kombe la mabara  2017 - kwa mujibu wa fifa viwanja vingine vitakavyo tumika katika kombe la mabara ni  Spartak Moskva's ,Kazan na  Sochi.
"

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers