HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

19 December 2012

Mario Balotelli AKUBALI KULIPA FAINI --; ULAYA KUCHIMBIKA KESHO



Ligi ya Mabingwa Barani ulaya  hatua ya kumi na sita mtoano   itapangwa kesho huko  Nyon saa tano Asubuhi kwa saa za mashariki ya kati   11.30CET Alhamisi   20 December –  ambapo mabingwa tisa wa michuano hiyo wakihusika . 

Bingwa mtetezi hatokuwemo lakini Malaga ambao wanaingia kwa mara ya kwanza pamoja na timu nyingine 15 ambazo zimewahi kucheza hatua hii zitawajibika  wakati Real madrid wanaingia mara ya kumi na sita mfulizo kwa timu zilizotwa ubingwa huo.
.
Mtaifa Tisa tofauti yanawakilishwa katika hatua hii na ni timu Tano tu ndizo zilizokuwemo katika hatua hii msimu uliopita : FC Bayern München, FC Barcelona, Arsenal FC, AC Milan na  Madrid. huku timu mbili tu zikiwa zikiwa zimeanza katika hatua awali za kufuzu kwa makundi  , Málaga na Celtic FC 

Washindi wa kila kundi watapata faida ya kuanzia ugenini huku wakipangwa kucheza na washindi wa pili  

WASHINDI WA MAKUNDI : Paris Saint-Germain FC (FRA), FC Schalke 04 (GER), Málaga CF (ESP), Borussia Dortmund (GER), Juventus (ITA), FC Bayern München (GER), FC Barcelona (ESP), Manchester United FC (ENG)

Washindi wa pili : FC Porto (POR), Arsenal FC (ENG), AC Milan (ITA), Real Madrid CF (ESP), FC Shakhtar Donetsk (UKR), Valencia CF (ESP), Celtic FC (SCO), Galatasaray AŞ (TUR)

Mechi za Mashindano hayo zitaanza  12/13 na  19/20 Mwezi  February wakati marejeano 5/6 na  12/13 March. hakuna timu zitakazo cheza zilipokua kundi moja wala za nchi moja shughuri itaendeshwa na  Katibu mkuu wa  UEFA  Gianni Infantino na Mkurugenzi wa Mashinadano wa UEFA  Giorgio Marchetti, akisaidiwa na balozi wa uefa  Na mchezaji wa zamani wa Liverpool   Steve McManaman.

Mario Balotelli AKUBALI KULIPA FAINI


Mshambulijai wa Manchester city  Mario Balotelli amefuta kesi yake mahakani dhidi ya klabu yake ya city baada ya kukubali kulipa faini ya mshahara wa majuma mawili kama adhabu ya kinidhamu dhidi yake kutokana na Takwimu mbaya ya Nidhamu msimu uliopita .

 Kesi hiyo ilitakiwa kusikizwa leo lakini kutokana na mazungumzo yaliyofanyika jana usiku kati ya pande zote mbili , Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 amefanya maamuzi hayo kama kumheshimu kocha mkuu wa klabu yake Roberto Mancini, na Mashabiki kwa ujmla ".

 "Mario ataendelea kuwemo katika mechi inayofuata dhidi ya Reading klabu hiyo" imesema
Mshambuliaji huyo aliipinga klabu yake kwa kumkata mshahara mara baada ya kukosa mechi 11 na za kimataifa  baada ya kukabiliwa na adhabu hiyo.

Mshambuliaji huyo alitarajiwa kwenda mahakani pamoja na Mwanasheria wake kutoka italia na mwakilishi kutoka chama cha wachezaji wa kulipwa huku City ilitarajiwa kuwakilishwa na wanasheria wa timu hiyo Mshahara wa wiki mbili ni adhabu sahihi kwa wachezaji wote wa kulipwa 

  City ilianza kumtuhumu mchezaji huyu Mara baada ya kupewa kadi nyekundu mechi dhidi ya arsenal mwezi April 2012  na alipewa kadi za njano Tisa na Nyekundu tatu katika msimu  mmoja .
MASHABIKI WA ZENIT ST PETERSBURG NI WABAYA NA WABAGUZI 

Mlinzi wa klabu ya Anzhi Makhachkala Christopher Samba. Amewatuhumu mashabiki wa klabu yake kwa kusema ni wabaya na wabaguzi na wanaishi katika karne nyingine kabisa na sio hii ya ishirini na moja , Mashabiki hao ambao hawataki kuona mchezaji mweusi na shoga wakizitumikia klabu za urusi ,Anasema "Sishwangazi sana , Kila mtu anajua kuwa  Mashabiki wa  Zenit sio wazuri  na ni wabaguzi . 

 "Wanaishi katika sayari nyingine Ni siku mbaya  katika soka ya Urusi aliongeza  : " katika wakati huu ambapo jamii tofauti katika nchi tofauti wanatengeneza timu . Kama hawawezi kukubaliana na hili basi kamwe hawataendelea ." 

 Zenit Ndio timu pekee iliyokuwa haina mchezaji mweusi mpaka pale aliposajiriwa Raia wa Brazil Hulk na kiungo wa Ubeligi   Axel Witsel. 

 Klabu iliwahi kupigwa faini ya Shirikisho  la soka la Urusi baada ya mashabiki kumrushia Ndizi mchezaji wa  Anzhi Makhachkala -na mlizni wa Kushoto wa klabu hiyo  Roberto Carlos kabla ya mechi dhidi ya Lokomotiv Moscow   March 2011. 

 Wachezaji weusi hupigiwa  miruzi ya kama ishara ya kumwita nyani  
  Samba amesema kuwa Tabia hiyo inaweza kuathiri maandalizi ya ya Kombe la Dunia mwaka 2018 kwani itakuwa ngumu kucheza hasa kwa timu kutoka afrika na za ulaya ambazo zinawachezaji weusi 

Benzema TUPO TAYARI KUPIGANA  MACHO YAPASUKE 

Mshabuliaji wa Real Madrid  Karim Benzema amewaonya Viongozi wa La liga   Barcelona kuwa timu yao haitaachana na mbio za ubingwa japokuwa wapo nyuma  kwa alama kumi na tatu baada ya kwenda sare na Espanyol  huku vijana wa  Tito Vilanova' wakiiibamiza  Timu inayoshika nafasi ya tatu  Atletico Madrid 4-1 katika Dimba la Nou Camp.

Kocha wa Madrid  Jose Mourinho alinukuliwa akisema kuwa  kwa vitendo haiwezekani kwa sasa kutetea ubingwa wa la liga huku Barca wakiwa wamepoteza alama moja tu Ni vigumu kwa Mabingwa Mara tisa wa ulaya kutetea taji hili tena na kupigana alama kumi na tatu hii ni tofauti kubwa sana  

,Kama hatuta Endelea kufungwa hatuwezi kukubali kuwaachia   Barça,wachukue kila hisi namna hiyo  . Benzema ALILIAMBIA Jarida la Kifaransa .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers