HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 December 2012

Sudan yawasilisha rufaa kwa CAS

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Sudan, limewasilisha rufaa kwa mahakama ya upatanishi ya michezo-Cas, kupinga uamuzi wa shirikisho la mchezo huo duniani FIFA, wa kuipokonya ushindi wake katika kinyang'anyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia, kufuatia tuhuma kuwa ilimjumuisha mchezaji ambaye hakustahili kuwepo katika kikosi chake.

Mahakama hiyo hii leo imetangaza kuwa inatarajia kutoa uamuzi wake kufikia mwisho wa mwezi Februari mwaka ujao, kabla ya michuano ya kufuzu kwa fainali hizo kuanza tena.

Sudan ilishinda Zambia kwa magoli 3-1 mjini Khartoum, tarehe mbili mwezi Juni mwaka huu, lakini FIFA, iliamua kuipa Zambia, ushindi wa mabao 3-0, baada ya kuamua kuwa Saif Ali, ambaye alifunga bao la pili, Kuwa halikuwa hatakiwi kuchezeshwa  kwenye mechi hiyo baada ya kupewa kadi kadhaa za njano katika mechi zilizotangulia.

Ali, alipewa kadi nyekundu wakati Zambia ilipoishinda Sudan katika mechi ya kufuzu kwa kombe la Mataifa bingwa barani Afrika, mwezi Februari.

Ikiwa Sudan itakabithiwa ushinda wake, itarejea tena kileleni mwa kundi lao mbele ya Ghana.

Lakini ikiwa mahakama hiyo ya Cas, haitabadilisha  uamuzi wa FIFA, wa kuipa Zambia ushindi, Zambia itakuwa imejizolea alama sita baada ya kucheza mechi mbili.

Sudan imepangiwa kuchuana na Ghana tarehe 22 mwezi Machi mwaka ujao nayo Zambia kupepetana na Lesotho siku hiyo hiyo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers