Huo
ni mchezo wa kwanza wa vilabu bingwa barani Afrika ambapo Simba
watakuwa wenyeji kabla ya mchezo wa marudiano utakao fanyika nchini
Angola wiki mbili zijazo.
Bi
Rahma amesema mchezo huo ni muhimu kwa Simba kwani watakuwa wakicheza
wakiwa katika uwanja wa nyumbani hivyo watakuwa wakihitaji matokeo
mazuri kabla ya mchezo wa marudiano.
Rahma
ambaye aliifandhili Simba ilipofanya ziara ya maandalizi kabla ya
kuanza mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, amesema
ameitembelea kambi ya timu ya Simba ilipokuwa Arusha na vijana wote
wameonyesha kuwa katika ari ya kufanya vizuri, hivyo basi wanahitaji
kupata sapoti ya mashabiki wake Jumapili uwanja wa taifa.
Amesema
mchezo wa soka siku hizi ni wa jinsia zote na kwamba wanawake kwa
wanaume wajitokezea kwenda kuipa nguvu timu yao ili iweze kupata matokea
mazuri bila kujali mapenzi ya vilabu kwa kuwa Simba ni mwakilishi wa
Tanzania.
www.rockersports.com/
No comments:
Post a Comment