HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 February 2013

GIDABUDAY KUCHAGIZA KILIMANJARO MARATHON JUMAPILI HII MKOANI KILIMANJARO

http://www.arushatimes.co.tz/2011/33/images/679/680%20Wilhem%20Gidabuday.jpg 

Mwanariadha  na mwanaharakati wa mageuzi katika michezo, Wilhelm Gidabuday amethibitisha kuongoza timu ya wakongwe wenzake katika mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Marathon yanayotarajia kufanyika jumapili ya Machi 3, mkoani Kilimanjaro.

Gidabuday amesema wameamua kuja Kilimanjaro Marathon mwaka 2013 kwa lengo la kuwaunga mkono wakimbiaji wa kitanzania na kuhakikisha kuwa mbio za mwaka huu hazirudii makosa ya miaka ya nyuma.

Amesema kuwa mbio za Kilimanjaro marathon ni mbio kubwa kuliko zote Tanzania na hivyo ni vizuri watanzania wakijionea ufahari wa kuandaa mbio kubwa kama hizi katika ardhi yao huku akiwashukuru waandaaji wa mbio hizi kwa jitihada zao kufanya mbio hizi kuwa za kimataifa zaidi.

 Amewataja wanariadha wakongwe atakaoongozana nao, wakiwemo wanaokimbia hadi hivi sasa, kuwa ni pamoja na Andrea Sambu ambaye aliwahi kuwa bingwa wa dunia pekee Mtanzania katika mbio za nyika za dunia mwaka 1991, Faustin Baha Sule, ambaye ni mshindi wa medali ya fedha mbio za nusu marathon 2000.


Wengine ni John Steven  Akhwari aliyeiwakilisha nchi katika mbio kadhaa za nyika za dunia, Getuli Bayo, Michael Sarwatt, Thadeo Nada na Anthony Mwingereza ambao kwa pamoja wamewahi kupeperusha vyema bendera la Taifa.
 







1 comment:

  1. Mimi naenda Moshi kumona huyu jamaa, ee bwana huyu mtu hatari lazima nimone, mwili kanyimwa lakini akili na ujasiri tele, namkubali sana akifuatiwa kwa karibu na Mike Wambura.

    ReplyDelete

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers