HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 March 2013

REKODI HII HAIJAVUNJWA KATIKA SOKA DUNIA NZIMA




 
Just "Justo" Fontaine (Alizaliwa Tar  18 August 1933 katika jiji la  Marrakech, huko Morroco ) Ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa anajulikana zaidi kwa rekodi pekee ya kufunga magoli mengi zaidi katika fainali moja za kombe la dunia    zilizo fanyika  Mwaka 1958 akifunga magoli 13
Ndiye mchezaji pekee anaye shikilia Takwimu hiyo ni moja kati ya wachezaji wanne ambao wamewahi kufunga magoli katika mechi moja

  

 Lakini Takwimu hii imevunjwa na mshambuliaji wa Brazil   Ronaldo De lima El fenomen , ambaye amefunga  magoli 15 lakini katika fainali Tatu  za kombe la dunia tofauti na fontaine ambaye alifunga kwenye fainali moja , Gerd Müller yeye  amefunga goli 14 katika fainali mbili na   Miroslav Klose  kutoka ujerumani  naye akifunga katika fainali tatu za kombe la dunia ambaye pia amefunga goli 14
Japokuwa ufaransa haikushinda kombe la dunia mwaka 1958 , Fontaine  amekuwa mchezaji wa pili kufunga katika kila mechi ya kombe la dunia baada ya  Alcides Ghiggia .
Japokuwa alizaliwa   Marrakech, alikwenda  Casablanca, na kujiunga na chuo cha  Lycée Lyautey.
Fontaine alianza kucheza soka ya ridhaa USM Casablanca, ambapo alichezea mwaka  1950 hadi  1953. Nice limchukua mchezo huyo na kumpa mafunzo ya soka mwaka 1953, na baada ya kupata mafunzo hayo alifunga magoli   44 katika msimu mitatu aliyochezea klabu hiyo  .
Mwaka  1956, alijiunga na Stade de Reims ambapo alikutana na mfaransa mwingine ambaye pia ni mzaliwa wa Moroco   Raymond Kopa, ambaye baadae alijiunga na Real Madrid mwaka  1958, Fontaine akauacha tabia yake ya kufunga  magoli kwani alifunga magoli  121 katika mismu sita akiwa na  Stade de Reims
Kwa ujumla   Fontaine alifunga magoli  165 katika mechi  200 za  Ligue 1, na  akishinda kombe  la nchi hiyo ; 1958 na  1960.
akiwa na jezo ya ufaransa , Fontaine' anaonekana kuwa bora zaidi  . katika mechi ya kwanza iliyochezwa Tar  17 December 1953, Fontaine alifunga mabao matatu pale ufaransa ilipoikung'uta  Luxembourg  mabao 8–0. katika miaka saba alifunga mabao 30 katika mechi  21 katika timu ya taifa . 

lakini yoote hayo , Fontaine atakumbukwa daima katika fainali za kombe la dunia mawaka  1958 FIFA World Cup kwa kuonyesha uwezo wa hali ya juu , kwa kufunga mabao  13 katika mechi sita tu —Huku mabao manne akiwafunga mabingwa watetezi Ujerumani Magharibi   na kwa wakati huo ilikuwa takwimu kubwa zaidi kuwekwa hasa ya magoli mengi katika mecho moja Takwimu ambayo haijafungwa mpaka Leo  . na ilimpatia ufungaji bora na kupewa kiatu cha dhahabu katika mashindano hayo .



Fontaine alicheza mechi yake ya mwisho mwaka  1962 Mwezi july , na alilazimika kustaafu soka akiwa na miaka  (28 na miezi kumi na moja   ) kwa sababu ya majeraha,japokuwa alirejea kiwanjani mwaka  1967, Lakini aliweza kucheza mechi mbili ambazo zote zilikuwa za kirafiki na waliishia kufungwa .
 Akiwa Mkufunzi wa soka wa  Morocco, aliiongoza timu hiyo ya taifa ya kushika nafasi ya tatu mwaka 1980 katika mashindano ya mataifa ya afrika  Badou Zaki, Mohammed Timoumi na  Aziz Bouderbala. Morocco iilikaribia kufuzu kombe la duni 1982   lakini ilifungwa na Cameroon.
 Pelé  ni moja katika wachezaji magwiji  125 ambao wako hai ambapo  March 2004 alipewa nafasi ya Kumtunuku kuwa mchezaji wa miaka hamsini iliyopita katika soka la Ufaransa baada ya shirikisho la soka la ufaransa kumpa heshima hiyo .

Mchezaji huyu aliwa kuandaliwa kipindi maalum cha runinga na gwiji la soka la uingereza Gary Lineker akimfanya mahojiano nae kuhusu maisha yake ya kandanda 
lakini katika mechi ya nusu fainali brazil ilishinda baada ya ufaransa kucheza wakiwa pungufu  katika dakika ya 36 mchezaji wa ufaransa Vava alitoka  baada ya kuumia mguu hakukuwa na sheria ya kubadilisha mchezaji kwa wakati huo na ufaransa ililazimika kucheza  pungufu kwa muda wote uliobaki   .  

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers