JE KUNA NAFASI ? ... Eden Hazard na Aaron Ramsey wanaweza kupambana tena .
Picture: RICHARD PELHAM
Wakuu wa ligi ya uingereza wanaumiza vidole vyao kwa kupiga mahesabu kwenye karatasi baada ya kuumiza kichwa sana kutafuta timu gani itafuzu hatua ya ligi ya mabingwa bila mechi za kufuzu kama klabu hizo za london zitamaliza zikiwa zimelingana alama na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa .
Hilo linaweza kutokea tu siku ya jumapili kama Gunners itashinda 2-1 dhidi ya Newcastle na Blues kutoa suluhu ya kutokufungana dhidi ya Everton.
kama mambo yatakuwa hivyo ,hakutakuwa na njia nyingine zaidi ya timu hizo kukutana tena — atakaye fungwa katika mechi hiyo atakuwa hana namna zaidi kucheza mechi kufuzu klabu bingwa ya ulaya na mshindi kwenda moja kwa moja katika hatua ya makundi katika michunano ambayo inavuta hisia za watu wengi,Mechi hiyo itakuwa ni ya kuvutia na bila shaka itaperekwa uwanja wa wembley ,Lakini tatizo sio hilo ni lini mechi hiyo itachezwa? .
Chelsea inatarajia kwenda kufanya ziara USA ambapo itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya
Manchester City wiki ijayo , wakati huo huo kukiwa na maechi ya kirafiki kati timu ya taifa ya uingereza mechi itakayo chezwa May 29 Dhidi ya Jamhuri ya Watu Ireland ikifuatiwa na Brazil June 2.
hakuna klabu hata moja itakayo kubali kucheza mwezi wa sita lakini mechi hii ni sehemu ya sheria ya ligi kuu ya uingereza .
Kifungu cha sheria kinasema hivi : “Kama ikiwa mwishoni mwa msimu ...shida ya nani kupata mshiriki ramsi katika mashindano halipata ufumbuzi kwa sababu ya klabu moja au mbili zimefungana alama au magoli ya kufunga , Klabu hizo zinatakiwa kucheza mechi moja zaidi au kucheza zenyewe katika uwanja ambao kila timui itakuwa ngeni .
“Mfumo , muda na Uwanja ambao mechi hiyo itabidi ichezwe utaamualiwa na bodi .”
No comments:
Post a Comment