HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

25 May 2013

AUREVOIR LIEWING KIBADENI NDANI

 
Baada ya kupiga chenga mara kadhaa huku blogu hii
ya Salehjembe ikiendelea kuandika kuhusiana na kufukuzwa kwa Kocha Patrick
Liewig.Blogu hii iliandika kuhusiana na mazungumzo ya
Simba na Kocha Abdallah Kibadeni, lakini uongozi ukasisitiza Liewig ndiye kocha
na wataendelea naye.Lakini leo, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseh
Itang’are ameweka mambo wazi kwa kusema Liewig ametimuliwa kazi na jukumu
amepewa Kibadeni.“Kibadeni ndiye kocha mkuu, tutamalizana vizuri tu
na Liewig, unajua sera ya Simba ni vijana na inaonekana Mfaransa huyo hataki
tena vijana.“Sasa tumeona aende tu na tuendelee na Kibadeni,
lakini tutamlipa haki zake zote ili tumalizane vizuri,” alisema Itang’are
maarufu kama Mzee Kinesi.Kwa sasa, Liewig, kocha mzee zaidi kuifundisha
Simba katika kipindi cha miaka zaidi ya 15, sasa yuko kwao Ufaransa kwa
mapumziko na hajui sakata la kufutwa kazi.
SALEHJEMBE .BLOGSPOT.COM (CREDIT)

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers