HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 May 2013

CHANETA KUTAFUTA KOCHA MPYA KUKUTANA CHANEZA JUNI MOSI


 

Chama cha mchezo wa netiboli nchini (CHANETA) kinatarajia kukutana Mei 31 kwa ajili ya kujadili uteuzi wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya netiboli inayojiandaa kushiriki mashindano ya ubingwa wa Afrika.

Mashindano hayo yanayoshirikisha timu za taifa kutoka nchi mbalimbali za Afrika yamepangwa kufanyika Juni mwaka huu nchini Malawi.


 Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Kibira amesema Taifa Queens inahitaji kocha mpya kwa sababu kocha Mary Waya amemaliza mkataba wa kuinoa timu hiyo tangu mwaka jana.


Kibira amesema jambo hilo linawalazimisha kukutana kutafuta kocha mpya.

  "makocha wapo wengi lakini lazima viongozi wote wakutane na kujadili nani anayesteahili kupewa timu hiyo".

Wakati huo huo, CHANETA inatarajia kukutana na chama cha netiboli cha Zanzibar (CHANEZA) kwa ajili ya viongozi kufahamiana ikiwamo kupanga mikakati ya kuendeleza mchezo wa netiboli nchini.
kikao cha pamoja kinatarajia kufanyika Juni Mosi mjini Zanzibar, ambapo wajumbe wote watahudhuri na kupeana mikakati ya kuinua mchezo wa netiboli.

"Tunatarajia kwenda Zanzibar kukutana na viongozi wa kule, lengo ni kudumisha umoja wetu kwa manufaa ya mchezo huu," alisema Kibira.

Vyama hivyo vimekuwa vikivutana kwa miaka mingi.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers