
ROBERTO MANCINI inaonekana kama kesho anaweza kupewa mkono wa kwaheri na klabu yake ya Manchester City baada ya kufungwa katika fainali ya kumbe la FA Cup dhidi ya Wigan.
Mtaliano huyu anaonekana anajua kinachoendelea baada ya kikao cha Bodi ya Timu hiyo kabla ya mechi yao katika uwanja wa Wembley.
Na inaonekana hata kama angeshinda mechi hiyo dhidi ya Latics bado isingetosha kuushawishi uongozi huo kumbakiza katika kikosi hicho mkufunzi huyo wa zamani wa Inter Milan .
Lakini sasa anaweza akafukuzwa kesho mapema , ambapo itakuwa siku moja baada ya kutwaaa ubingwa mwaka jana .
Mancini, 48, anatarajiwa kupokezwa na kocha wa Malaga’ raia wa chile Manuel
Pellegrini — Muda mchache baada ya klabu hiyo kutangaza kuwa itakwenda kufanya mazoezi kwa ajiri ya msimu ujao huko New York .
Kabla ya kwenda huko Mabingwa hao wa mwaka jana wana mechi mbili ambazo ni kati ya Reading siku ya Jumanne na jumapili dhidi ya Norwich .
Mancini atakuwa bado mkufunzi wa Timu hiyo mpaka pale ambapo watamaliza majadiliano ya kandarasi aliyoingia miaka miine iliyopita .
Kama atakufukuzwa kabla ya Mechi hizo kaimu kocha wa Timu hiyo Brian Kidd ataingoza timu hiyo ambayo inahitahiji alama moja kujihakikishia nafasi ya pili nyuma ya united
Akiongea baada ya Mechi waliyopoteza Dhidi ya Latics, Mancini "Nitajua Mustakbali ndani ya majuma mawili yajayo ".
Aidha amewatuhumu maafisa wa klabu yake kuwa wameshindwa kutunza siri kuwa nafasi yake itachukuliwa na Pellegrini baada kuonekana kuwa na jamabo kama hilo mwezi February.
Tetesi zinasema kuwa kulikuwa na dalili kuwa baada ya fainali ya Kombe la FA kocha wa zamani wa
Real Madrid atachukua nafasi katika dimba la Etihad baada ya kuoneka kuna asimilia ndogo ua mkufunzi huyo kuhamia timu hiyo .
Na ijumaa iliyopita ,Taarifa zilisema kuwa Mkurugenzi wa soka wa timu hiyo Txiki Begiristain amekubali Pellegrini kuchukua nafasi kwenye timu hiyo.
No comments:
Post a Comment